Taarifa zilizotufikia hivi sasa ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
amekatisha ziara yake wilayani Mbozi na alikuwa njiani kurudi jijini Mbeya kukutana
na wamachinga waliouteka mji tangu asubuhi. Kinachosubiriwa ni iwapo wamachinga
hao watakubali kuongea naye kwani walishatamka kuwa hawataki kumuona.
Muda huu machinga walikuwa wakilazimisha kuingia katikati ya jiji kushinikiza
kuachiwa kwa wenzao wanaoshikiliwa na polisi
Chanzo:Mbeya Yetu Blog |
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake