ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 15, 2011

Simba wa Cameroon wagoma

Timu ya Taifa ya Cameroon
Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon wamegoma kusafiri kwenda kucheza mechi ya kimataifa kutokana na mzozo wa kifedha.
Mchezo wao dhidi ya Algeria, uliopangwa kuchezwa siku ya Jumanne umefutwa kutokana na hilo.
Mzozo huo ulizuka baada ya timu hiyo kucheza mechi mbili dhidi ya Morrocco na Sudan mjini Marrakesh. Marupurupu kwa ajili ya michezo hiyo haikulipwa na wachezaji wakaamua kugoma kwenda Algeria.
"Tatizo la malipo lilitajwa wiki iliyopita na hakuna suluhu iliyopatikana," wamesema wachezaji hao kupitia taarifa waliyotoa.
"Timu ilicheza kwa moyo na kwa madili ya kimichezo mjini Marrakesh, lakini tumeamua kutokwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa Novemba 15.
"Wachezaji wa timu ya taifa wanasisitizia utaifa wao na kutoa wito kwa mamlaka za soka za Cameroon kutimiza ahadi zao kwa wachezaji."
Mzozo huo ni tatizo kubwa kwa kocha mpya wa Simba hao Denis Lavagne, ambaye alichukua nafasi ya Javier Clemente aliyefukuzwa kazi mwezi uliopita.

No comments: