TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars jana ilijiweka katika mazingira mazuri ya kuingia hatua ya makundi katika kinyang'anyiro cha kuwania kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Chad.
Habari kutoka N'Djamena zinasema mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Stars ilicheza vizuri karibu katika muda wote wa mchezo.
Stars ndio ilianza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 11 kupitia kwa mshambuliaji wake, Mrisho Ngassa.
Lakini bao hilo halikudumu kwani dakika moja baadaye Chad ilisawazisha bao hilo kupitia kwa A. Labo.
Iliilazimu Stars kusubiri mpaka dakika 10 kabla ya kumalizika mchezo ndipo iandike bao la ushindi kupitia kwa Nurdin Bakari.
Kwa ushindi huo, Stars imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi kwani sasa inahitaji sare ama ushindi wowote katika mechi ya marudiano itakayochezwa Jumanne ijayo ili kufuzu hatua hiyo.
Matokeo mengine katika mechi zilizochezwa jana, Msumbiji ambayo ilikuwa ugenini visiwa vya Comoro imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, na Namibia ilitamba ugenini kwa kuichapa Djibouti mabao 4-0.
Rwanda iliibana Eritrea na kutoka nayo sare ya bao 1-1, Kenya imetamba ugenini Shelisheli baada ya kuwachapa wenyeji mabao 3-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeipiga Swaziland mabao 3-1.

No comments:
Post a Comment