ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 14, 2011

Symbion kuingiza megawati 60 za umeme gridi ya taifa mwezi huu

Takriban megawati 60 za umeme wa kampuni ya Symbion unatarajiwa kuongezwa kwenye gridi ya taifa mwishoni mwa mwezi huu ikiwa ni katika juhudi za kusaidiana na serikali kukabiliana na tatizo la nishati hiyo hapa nchini.
Tayari vifaa kwa ajili hiyo vimewasili nchini kutoka Dubai na ufungaji wake unaendelea Dodoma.
"Kazi ya ujenzi wa mtambo huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu," Mratibu wa mradi wa kampuni ya Symbion Dodoma, Don Brindle, aliwaambia waandishi wa habari waliotembelea eneo panapojengwa mtambo huo wa megawati 60.

Vifaa hivyo viliwasili nchini siku kadhaa zilizopita.
Brindle alisema kampuni yake inataka kuweka mitambo hiyo haraka iwezekanavyo ili kukabiliana na tatizo la umeme nchini.
Kwa mujibu wa afisa wa Symbion, kampuni hiyo ya Marekani tayari pia imeongeza megawati 37 katika mitambo yake ya Ubungo kwenye gridi ya taifa na sasa itaongeza megawati 60 mwishoni mwa mwezi huu Dodoma.
Brindle alisema mtambo mwingine wa megawati 145 wa kamouni ya Symbionunatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao hii ikimaanisha kwamba kutakuwa na nyongeza ya megawati 242 tangu kampuni hiyo ilipoanza kuendesha mitambo yake ya Ubungo.
Ikiwa ni moja wa washirika muhimu katika pango wa serikali wa mpango wa dharura wa umeme, Symbion imepewa mkataba wa kuchangia megawati 205.
Washirika wengine katika mpango huo ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Aggreko.
Meneja wa Symbio wa mradi huo wa Dodoma alisema: Kusema kweli Symbion imechukua hatari nyingi za kibiashara kuwasadia Watanzania, Shirika la Umeme nchini (Tanesco) na Wizara ya Nishati na Madini. Hakuna kampuni binafsi ingefanya hivyo," alisema.
Brindle alisema: Symbion haiwezi kulipwa kabla mkataba haujathibitishwa lakini imekwenda mbele zaidi na ujenzi licha ya hilo."
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Symbion, Paul Hinks, alisema Serikali ya Tanzania na Tanesco iliitaka Symbion kusaidia kuondoa tatizo la umeme hapa nchini na "tulikubali kwa changamoto hii na nafikiri matokeo yake yaanza kuonekana sasa."
Alisema ongezeko la megawatti 60 Dodoma mwishoni mwa mwezi huu, kutaboresha upatikanaji wa umeme na megawati 145 zitakazowekwa Desemba, mwaka huu, kutaleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya wananchi.
CHANZO: NIPASHE

No comments: