ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 11, 2011

AFISA WA TCRA ASHINDA TUZO UINGEREZA

 Afisa Semu Mwakyanjala
Baraka Baraka Akifanya Mahojiano na afisa Semu 
Kutoka Kushoto Naibu Balozi Chabaka, Semu na Tim
 Mh Naibu balozi akitafakari Jambo
 Picha ya Pamoja Mh Balozi Kallaghe, Tim, Semu Naibu Balozi Chabaka na Allen
 Tim Hunt na Frank Eyembe
Tim Hunt Reginal Manager Africa & Middle East
Wakati wa kuazimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania hapa Jijini London Ubalozi wetu katika siku ya Ijumaa Tarehe 9 Desemba 2011 ulipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.

Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote  kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.

Asanteni,

URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na Miss Jestina Blog

No comments: