ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 14, 2015

MREMA ASEMA UKAWA UMEPOTEZA MWELEKEO

Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha TLP , Augustino Lyatonga Mrema

Mwenyekiti wa taifa wa TLP Augustine Mrema amewatahadharisha watanzania kuwa macho juu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao umepoteza mwelekeo na kuyumba kisiasa na kudai kuwa hawafai kuingia ikulu na kuongoza nchi.
Mrema ametoa tahadhari katika eneo la njiapanda baada ya kurejea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Moshi kuchukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Vunjo huku akisindikizwa na wafuasi wake.
Amesema, kitendo cha ukawa kumkashifu hadharani waziri aliyestaafu Mh

Edward Lowasa kuwa ni fisadi na baadaye kumpokea na kumteua kuwa mgombea wa urais ukawa imeonyesha udhaifu mkubwa na kwamba watanzania wa sasa si wakuburuzwa.
Mh. Mrema amesema kuwa haiwezekani mtu alieachwa na chama na kuonekana hafai kutokana na tuhuma za ufisadi kicha CHADEMA ndio wakaona anafaa kuwa mgombea huko ni kuonyesha kutokuwa na msimamo ndani ya hivyo ni vigumu kuwapa uongozi wa nchi

11 comments:

Anonymous said...

CCM B huyu

Anonymous said...

Mheshimiwa Mrema ni vyema ukabakia kimya na TLP yako na uwe ukijua wazi jimbo la Moshi haliwezi kurejea kwako ndio tunakaribia kukusahau kwenye ulingo wa kisiasa. Wewe ulikuwa mmoja wa wapiganaji wa njiabhiyo ila ulikosea kidogo kwani CCM bado walikutumia. Huyu kaamua wakati muafaka unalionaje hilo bora na wewebungerudi CDM auCCM.!!pole hii ni moja kwa moja hakuna kusimama.

Anonymous said...

Ndg Mrema unayosema yana dira kwa waTanzania? Au na wewe umeamua kuiua Demokrasia nchini. Wewe ni mpinzani kwelinau ndio walewale kina Lipumba.?

Anonymous said...

Huyu Mzee Lyatonga alikuwa mwanasiasa moto enzi zake lakini kwa sasa amekwisha kabisa kisiasa, kwisheney...sawa na mlalahoi, anachumia tumbo na kujaribu kuganga njaa. Jimboni kwake hatakiwi tena anadhani kwa kujikomba anaweza kupata chochote tena kutoka CCM. Akiitisha mkutano hata watu 100 inakuwa vigumu kuwapata. Kama UKAWA wamekosea kumchukuwa na kumsimamisha Lowassa kama mgombea wao, wanainchi wataamuwa kwenye sanduku la kura hiyo tarehe 25 Oktoba.

Anonymous said...

Mzee kaa pembeni, we mwenyewe tiketi yako imewaka engine light. Muda wa nyota ingine kushamiri. Sasa unamaana CCM ndio wana mwelekeo kisa uko kwenye payroll au? Watu wengine bwana kama huna cha kusema we rudisha fomu yako kwa njia ya posta hamna mtu atasema lolote. Na kwanza ulisha save save maana this term, thats it. Kwishneee mzee wangu inabidi tukalime tu Vunjo na kupiga porojo huku movie ikiendelea.

Anonymous said...

Mhe. Mrema, sera zako hazina mshiko zimepitwa na wakati. Umepata nini huko CCM? Si wewe yule Mrema uliyekuwa unaipiga vita ccm miaka ya 1985? sasa umekuwa rafiki wa ccm? Mungu akubariki. TLP ndio haina mshiko. Kwani TLP ndio nini? Je umewaona wafanyakazi wanavyonyanyasika na ccm? Sasa mbona hujafanya lolote. T....Labor......Sijawahi kuona sera zako zikielekeza kuhamasiha watu wapate ajira njema, wala chochote chenye uhusiano na LABOR!

Anonymous said...

Hivi kuna watu bado wanamsikiliza Mrema? Huyu ndiye kati ya walioharibu Demokrasia, mwingine ni Ibrahim Lipumba, akiwa na UKAWA/ au kwenye chama chake anaongea kama kusapoti, akiwa miaikitini anatetea serikali ya Kikwete, police wakimpiga analaani CCM lakini baadaye anarudi huko huko. Kweli kusoma sana si kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri.

Anonymous said...

Hiyo kofia ndiyo imepoteza muelekeo

Anonymous said...

Huyo mjamaa hata kiingereza kinampiga chenga. Huko aliko hata ss tumeishi na kufanya kazi sana huko....mbona tu naenda kwenye msiba ya rafiki zetu, tena hao hao wazungu, bila kukaribishwa?

Anonymous said...

Bwana Mrema tafadhali wasiliana na bwana Lipumbu mnaweza kuwa pamoja upinzani wenu mnafanana, usihubiri dini usiyo ijua endelea na agano la kale sisi tuna agano jipya"ukawa" chukueni hela za ccm tunacho waomba kura zenu tu mnaweza kutupigia sisi tunaelewa maisha sio mchezo Tanzania.

Anonymous said...

Kuna kuchoka akili hadi mwili
Baba mrema kuchoka vyote anatisha