Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe amesema kuwa hawatashiriki shughuli ya kuapishwa kwa Dk. John Pombe Magufuli inayotarajiwa kufanyika Alhamis, Novemba 5, 2015.
Kauli hiyo ya Mwenyekiti Mbowe aliyoitoa leo, imekuja wakati kukiwa bado kuna sintofahamu kubwa miongoni mwa Watanzania kuhusu mchakato wa uchaguzi hususan upigaji kura, ukusanyaji na ujumlishaji wa matokeo ulivyofanyika hasa katika nafasi ya urais.
"Hatutahudhuria shughuli hiyo ya kumwapisha Magufuli. Tumekubaliana wote kwenye UKAWA, ndani ya CHADEMA, viongozi wetu, wabunge wetu wote hawatahudhuria uapishwaji wala sherehe.
"Tumetoa wito kwa wananchi wote, Watanzania wote, wapenda mabadiliko na wapenda haki wote kwa ujumla kutohudhuria shughuli hiyo," amesema Mwenyekiti Mbowe.
Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa UKAWA, wapenda mabadiliko wote na Watanzania wapenda haki hawakubaliani na wanapinga mchakato wa uchaguzi hususan matokeo ya urais ambayo, kwa mujibu wa Katiba ya Nchi aliyosema ni mbovu, yakishatangazwa hakuna haki ya kuyapinga katika mahakama yoyote ile.
"Tunataka nchi na dunia nzima ijue wazi kuwa hatukubaliani na mchakato wa uchaguzi hasa matokeo ya urais ambayo kwa mujibu wa Katiba yetu mbovu, Mwenyekiti wa Tume akishatangaza hakuna mahali pa kuyapinga."
"Matokeo ya ubunge au udiwani yanaweza kupingwa mahakamani, lakini kwa matokeo ya urais Katiba yetu mbovu inawafunga mikono na miguu Watanzania wote ambao wangependa waone haki imetendeka katika nafasi hiyo," amesema Mwenyekiti Mbowe.
"Watawala wamechezea haki ya Watanzania kupiga kura. Kura zimehesabiwa kama karatasi za kawaida tu. Hujuma dhidi ya matokeo ya wagombea wetu imehujumiwa waziwazi. Safari hii hujuma hazikuwa kificho tena. Kila mtu amejionea matokeo yaliyokuwa na Jaji Lubuva si yale ambaye yalikuwa yamebandikwa vituoni. Hayakuwa na uhalisia na matokeo yaliyokusanywa na mawakala. Uchaguzi umefanywa kama ni jambo lisilokuwa na maana yoyote. Hiyo ni hatari sana kwa taifa lolote linalotaka kukuza demokrasia kama mojawapo ya nguzo za maendeleo. Hatuwezi kukubali kufika huko," amesema Mbowe.
Aidha, Mwenyekiti Mbowe ameongeza kusema kuwa vyama vinavyounda UKAWA vimeitisha kikao cha Wabunge wateule wote wa vyama hivyo ambao watakutana Alhamis, saa 4 asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Imetolewa leo Jumatano Novemba 3, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
9 comments:
Blah!blah blah blah! Sisi waafrika tunalaana Kuna mwafrika kweli anaeshindwa uchaguzi akakubali kiroho safi bila kuleta mizengwe?
Mnasema uchaguzi si wa haki kwa sababu katiba iliosimamia uchaguzi sio nzuri sasa kwanini mlishiriki huo uchaguzi ? Sasa baada ya kushindwa ndio katiba sio nzuri? Nyinyi ukawa hasa chadema mnajulikana kabisa ni watu wa vurugu hamna sera, sera zenu ni vurugu na vitisho kwa serikali na wananchi. Angalau hao act wazalendo wanasera. Kwa hivyo kugoma kwenu kuhudhuria sherehe za kuapishwa raisi hazitaasiri kitu chochote kwani nyinyi ndio mnayohiihitaji CCM na serikali yake kwa hivyo msiende kabisa katika sherehe kwanza mnaogoga aibu na watu wangewazomeeni kweli kweli bora mnavyojifungia milango na hakuna mtanzania atakaefuata maelekezo ya kipuuzi kutoka kwenu ya kutoka huzuria sherehe kwani tayari watanzania mbali mbali kwa maelfu kutoka mikoani wapo daresalam kwa wakisubiria sherehe hiyo kwa hamu kubwa. Na tunawaomba watanzania ili kujiepushia aibu na kuliepushia taifa aibu na kuhakikisha Tanzania inasonga mbele tayari sasa umefika wakati wa kuikataa chadema kwanza imeshapoteza sifa ya sifa ya kuwa chama makini. Kitendo cha kumfukuza Dk Slaa na kumkumbatia mtu ambae kwa kauli yao wenyewe kuwa ni fisadi papa lowasa. sasa kwanini tena watanzania tuendelee tukubali kutapeliwa na hawa matapeli wa siasa?
Jaji Lubuva umeamua kuipeleka Tanzania pa h ali pabaya na umri ulio nao na dhamana uliyokabidhiwa. Haikitarajiwa ukubalinkusoma matokeo yasiyo rasmi badala yake umepokea yale yaliyoandaliwa na JM na timu yake. Uhalisiabwa Demokrasia umeuua wewe na timu yako ya Mh Rais.
Mbowe unapoteza Muda wako. Usiwafanye watanzania wajinga kwa maslahi yako. Hakuna utakalo fanya kuzuia au kuharibu chaguo la Watanzania. Chama chako kutoshinda isiwe sababu ya kudanganya umma kuwa kura ziliibiwa. Wasimamizi wote wa kimataifa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wahaki. Kazana kujenga chama chako na siyo kulalama. Utake usitake Magufuli ni Rais wako. Tii mamlaka ya nchi vinginevyo unajitafutia matatizo. Muhimu acha kudanganya vijana wet ambayo future yao bado ni tete. Watasota rumande pindi wakitoka itakuwa too late. Ndiyo majambazi watakao Kuja kukupiga risasi getini kwako. PLEASE STOP THE STUPID MOVEMENT.
Kwani walipokubali kushiriki katika Uchaguzi Mkuu, walikuwa hawalijui jambo hilo?
UKAWA, acheni kujiaibisha mbele ya dunia, jamani>
Je, kama Lowassa angechaguliwa kuwa raisi wa amamu ya tano, Chadema na Ukawa bado wangelalamika kuwa Katiba ya uchaguzi wa raisi nchini Tanzania ni mbovu ?
Vyama vya Chadema/Ukawa nadhani sasa vimefikia kikomo cha kuitwa vyama vya siasa kwani vimekuwa sawa na makundi ya wahuni yasiyo na mpangilio wowote wa manufaa kwa wananchi zaidi ya kueneza vurugu na wasiwasi usio kifani. Haya maelezo yao kuwa katiba ya nchi ni mbovu kwa ajili haiwaruhusu kwenda mahakamani kulalamikia kushindwa kwao kwenye uchaguzi wa rais ni upuuzi mtupu. Vyama hivi vimekuwa na wabunge walio kuwa wanahudhuria bunge kwa miaka mingi huko nyuma, kama swala hili ni tatizo kwa nini hawakuli hoji katika vipindi vilivyopita badala yake wanakuja kutuletea mizengwe leo baada ya Wananchi kuamua kutomchagua mtu wao? Waende au wasiende kwenye hafla ya kumtawaza Dk. Magufuli ni chaguo lao na wala sisi Watanzania wengi tunaoipenda nchi yetu na tunaitakia amani na mambo yote mazuri hatutaendeshwa na mawazo finyu ya viongozi wa vyama hivi na badala yake tutaendelea kuiunga serikali yetu na kumpa kila aina ya ushirikiano Rais wetu mpya katika harakati zake za kutuletea maendeleo. Naomba Watanzania wenzangu kuenda kwa wingi huko uwanjani kesho ili kuungana na Dk. Magufuli katika sherehe ya kuapishwa kwake.
Kinachotumaliza watanzania ni ushabiki wa kisiasa usio na miguu wala kichwa. Inabidi tufike mahali tuweze kujitambua, ndiyo Ukawa wana makosa yao walijua wazi kwamba tume ni ya sisiemu na bado wakashiriki uchaguzi. Walitakiwa kuyawaza haya kabla!!!!!! Lakini hii pia haitufanyi majuha kalulu kiasi cha kuacha kuona vitendo vya hujuma za wazi wazi zilizofanyika wakati wa uchaguzi. Kwenda au kutokwenda kwenye sherehe leo ni uamuzi wa mtu binafsi na si wa mbowe na ukawa yao lakini je, walichofanya watawala wetu mwaka huu ndiyo maana ya demokrasia. Naamini mtu yeyote mwenye akili timamu lazima alione hili na kulizungumzia kwa mapana na marefu. Weka ushabiki pembeni na weka maslahi ya taifa mbele. Tunaelekea wapi???????? Haya mambo tunatakiwa tuyaone sasa kabla ya uchaguzi mwingine na kushuhudia tukigeuka mazuzu tena. Kuna haja gani ya kwenda kupiga kura wakati unajua kura yako haiendi popote inaishia tuu wewe kupakwa wino.
Kwakweli uwe Ukawa au CCM hatuna budi kupongeza upinzani (Mbowe and co). Wameweza kuwaonyesha watanzania wengi weakness na uzembe mwingi unaotakiwa kufanyiwa kazi Mfano katiba. Kama katiba ime-ku favor leo in the future itakuumiza wewe au kizazi chako. Nafikiri King unge, Lowassa and co ni washahidi wa hili. Katiba waliyoikumbatia for years imekuja kuwaumiza wao. Ni muhimu kuweka maslahi ya nchi mbele na sio chama. Watanzania tujifunze uzalendo na sio ushabiki wa vyama. Let us call a spade a spade. Katiba tulionayo ya mwaka 77 ni ya chama kimoja. Hatuwezi ku-practice multiparty system chini ya katiba hii..plain and simple. Ata kwa CCM wenyewe Katiba hii haifai. Katiba ya kijamaa wakati vi ongozi karibia wote wana-practice capitalism?
Dolour!
Aibu kwa vyama vya siasa visivyo na viongozi wenye "guts" za kuwania wadhifa wa urais; wanabaki kuazima au kuchamaifya viongozi waliotupwa kutoka kwingine! Yafaa mjiuzulu na kuwaachaia wenye uwezo sio kufanya vyama kama kampuni binafsi.
When shall this political leadership mediocrity end?
Post a Comment