ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 30, 2015

Je, unadhani nini hasa chanzo cha umaskini Tanzania?


Tanzanite, Dhahabu, makaa ya mawe, almasi, urani, Mbuga za wanyama kama vile serengeti, Manyara, Ngorongoro, ardhi yenye rutuba, Mlima Kilimanjaro, maziwa makubwa matatu, bahari ya hindi na utajiri mwingine mwingi, hivi vyote vinapatikana ndani ya Tanzania lakini ajabu wananchi wake wengi ni maskini sana.

18 comments:

Anonymous said...

Ni vyema ukaulize Serikali zilizokaa na kupita ngwe ya miaka kumi. Wametumia kiasi gani na wamesaidia kiasi gani kwa wapiga kura wake. Swali kama hili linagonga vichwani mwa walala hoi..

Unknown said...

Hakuna cha kufikiri kuhusiana na chanzo cha umasikini Tanzania viongozi wasiowaadilifu kama wakina lowasa ndio chanzo kikubwa cha umasikini Tanzania.

Anonymous said...

CCM

Anonymous said...

Umasikini unaletwa na watu kutokuwa wabunifu na si chama wala serikali. Naishi nje ya nchi, wenzetu huku wanajituma na hawadharau kazi. Ubunifu ni wa kufikiria jinsi ya kujiongezea kipato, wenzetu hawana cha mjomba wala shamba la kuchuma matembele ya kula jioni, uvivu wako wa kufikiri una maanisha maisha yako yatakuwa ya tabu, hivyo watu wana biashara hata za kufyeka majumbani, bustani na kazi sie watz tunaziona hazina maana na wanazithamini na kuzifanya kwa bidii, na wanafanikiwa kimaisha.sie watz tunataka serikali itufanyie nini? Shule zipo, elimu uliyoipata kama haikufikirishi utakaa ukilaumu serikali zote zitakazokuja madarakani. Sijui nani katuloga.

Anonymous said...

ni uvivu wa kuchapa kazi,kukosa maarifa,kusubiri kufanyiwa kazi bila kutumika.mbona wengine wameweza why no us?tatizo la wengi ni kuitegemea serikali kwa kila kitu.kupeleka mtot shule -serikali,kubuni cha kufanya na kuthubutu-serikali,kufanya kazi kwa bidii na uaminifu -serikali,uzaendo kwa nchi yako serikali,kila kitu serikali where is your plypart?thats when the so calld umasikin unapotujia

Anonymous said...

Mafisadi.

Anonymous said...

Namba 2 unatia aibu. Hivi ile ripofi ya CAG uliisoma na mgawonwa ESCROW aligawa Lowasa! Kama una chuki ya Lowasa basi endelea kuiona CCM ndi baba yako ndugu zako wanakufa masikini na wewe huna mfano.

Anonymous said...

viongozi wanaongozwa na mfumo,nchi hii kwa miaka yote tangu uhuru tulichagua mfumo mbovu wa ujamaa historia duniani iko wazi sasa kuwa mfumo huu haukufaa wala hautofaa ikiwa lengo ni kuleta maendeleo kwa wananchi wa taifa lolote lile.

Tumejikita kwenye amani na kuongea lugha moja ya kiswahili kuwa ndio faida kubwa ya uhuru na kujitegemea kwetu, tumesahahu hayo mawili pekee juu ya umuhimu wake hayaondowi njaa,maradhi au kuleta miundo mbinu bora pamoja na elimu inayo hitajika katika kuleta uchumi unaohitajika,ni lazima kuyafahamu makosa haya ili tuweze kuleta mabadiliko kuendelea kutumia amani kama kigezo cha maendeleo peke yake matatizo sugu kama umeme,maji,ajira,afya na uongozi mbovu wa ccm utatumaliza siku zote.

hakuna kosa wala sio dhambi kukubali ukweli kuwa mfumo wa ccm ni mbovu kwa taifa hili tajiri katika mali asili,ujangiri wa mali za umma unaofanya na viongozi walio jitajirisha kama viongozi wa nchi tajiri ya Saudi Arabia kumbe ni viongozi wa nchi masikini kama yetu ni wa kushitusha,wananchi wa taifa hili hawana sababu ya kukipigia kura chama kinacho waibia mabilioni huku kikiwaahidi maendeleo kila uchaguzi.

sikustaajabu pale mkapa alipowaita wanaokipinga chama chake wapumbavu na malofa kwa sababu kama sio upumbavu wetu majangiri kama hawa wasingeliweza kujiuzia migodi,majumba na mabenki huku wakijikopesha mabillioni wakati wao wakiwa madarakani huu ni ukosefu wa nidhamu za mali ya umma na kiburi kilicho vuka mpaka.

nina hakika mwalimu angelikuwa hai asingekipigia kura chama alicho kianzisha,alituwekea mfumo wa ujamaa ambao sasa tunaelewa kuwa haukuwa na maana kwa tafa letu kwa sababu unapo taifisha kila kitu kwa kasi ile unaangusha uchumi wa taifa kwa kasi hiyo hiyo lakini mwalimu alikuwa na nidhamu na hakutuibia hata senti tano sasa kwa nini sisi tunao muenzi,kumheshimu, kumpenda tumpigie kura mgombea wa ccm tatizo sio chama au mtu ni MFUMO.

MDAU.
MOROGORO.

Anonymous said...

Ndg yetu unayejiita Sallenn! Hivi kweli unadhani au ni ile hulka ya wengi kuona Lowasa ni mbaya hivi Serikali hii iliyojiwekea madaraka miaka nenda na wanalindana kwenye ulaji, Ufisadi uliokidhiri na utajiri wa hali ya juu kama kina RW1 watoto wa majuzi na vituo vya mafuta kila mkoa na njiani! Wewe una nini hapo ulipo ndg zako nao wanaishi maisha ya njaa yote ni hii serikali wewe nawe unaona lakini unafumba macho au una ndg yako ndani yake unaogopa maisha ya baadae kwani wamezoea kuiba!!.

Anonymous said...

CCM na TANU ndizo tatizo. Wanajinufaisha wenyewe ndiyo maana wanapigana vikumbo kutafuta uongozi. TANU ilikuwa na sera chafu isiyotekelezeka ilikuwa imejaa watu wasio na ujuzi na wenye uelewa wa uchumi. Hakuna lingine na kwa chama hiki na kwa mwendo wake itachukua miaka mia moja ili angalau tufanane na wengine.

Anonymous said...

Chanzo cha umasikini inatokana na viongozi wenye madaraka kuwa wabinafsi sana na kuwa mafisadi na kujilimbikizia mali wenyewe.

Anonymous said...

CCM

Anonymous said...

viongozi kama lowasa, change,rostam Aziz, kingunge, list goes on and on.

Anonymous said...

Tunawakilishwa na viongozi na matajiri wachache wanaonufanika na rasilimali zetu.Kila mtu pamoja na bubu na viziwi wanajua kuwa nchi inamalizwa na wachache. Tujiulize vitalu vya mafuta waliouziwa ni kinanani na je serikali inaweza kuweka majina yao wazi?Vibali vya kuwinda wanayama ni nanai wamepewa na pia serikali ipo tayari kuweka wazi?Machimbo ya Almais, dhahabu,na gas je?Angalia wachina walivyo jaa hata mahindi wanauza je hawa ni wawekezaji?Kwanza hawa wachina wanaokuja hapa kwetu ni wafungwa wameambiwa kuwa wasirudi kwao ni kama wapo probation.Raia wa nje wanapata vibali vy kununua viwanja na ardhi bila ya kujali chochote.Angalia majirani zetu wa Kenya, mtanzania huwezi kununua kiwanja bila ya kuwa raia. umaskini ni kwa raia wa kawaida lakini viongozi wa serikali na mawaziri wote ni matajiri na hawajui kitu chochcote kuhusu mlalahoi.

Anonymous said...

Mfumo wa chukua chako mapema, mifumo wa upendeleo wa ccm, mfumo wa wizi wa rasilimal. Mfumo wa mtu kujiona yuko juu ya sheria!!

Anonymous said...

Kuchimba madini hakumsaidii MTU wa chini kuinuka . swali limekaa kiupotoshaji. Kuwa na madini hakutoshi.

Anonymous said...

Chanzo cha ukombozi ni fikra nzuri,elimu bora, na afya nzuri.

Anonymous said...

Bahati mbaya Lowassa haingii Ikulu labda miaka 80 ijayo.