ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 15, 2014

TANZANIA DIASPORA USA WAKUTANA NA MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA, MHE. JOHN SITTA,

  Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba na Waziri wa Afrika Mashariki​​, Mheshimiwa Samweli Sitta akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wanajumuiya wa New York na New England walipokutana jana Jumamosi June 14, 2014 mjini Boston, Massachusetts kumsalimia Mheshimiwa sitta na kumwelezea masuala ya Wanadiaspora likiwepo suala la uraia pacha. Baadhi ya Viongozi ni Mheshimiwa Sangiwa, M/Kiti wa New England, Mheshimiwa Mhella, Katibu wa New York, Dr. Temba, Mweka Hazina Msaidizi wa New York, Wanachama Mkereketwa, Akida na Chemi, pamoja ni viongozi wengine wa New England.
 Mheshimiwa Sitta akifafanua baadhi ya masuala aliyopata kuulizwa na viongozi wa Watanzania New England na New York hasa likiwemo suala la uraia pacha. Amewataka wanadiaspora wasiwe na wasiwasi kwani suala hilo litaletwa Bungeni na kujadiliwa wakati wake utakapofika.
 Mheshimiwa Sitta akisiliza maelezo ya viongozi kutoka New York na New England​​
 Mheshimiwa Sitta akiwa na Katibu wa New York, Mhella na Mweka Hazina Msaidizi wa New York, Dr. Temba​​
 Mheshimiwa Sitta akiwa na Mwenyekiti wa New England, Eliamani Sangiwa na Da Chemi Chemponda.​​
 New York Team in the house
Mheshimiwa Sitta akiwa mwingi wa furaha baada ya kuzungumza na viongozi wa New England na New York. akipungia na kuondoka na sisis tukasema  Karibu tena Mheshimiwa Sitta

26 comments:

Anonymous said...

mbona watanzania wenginewe hatujulishwi kukutana na mheshimiwa sitta mnakwendaga wenyewe au ndo mikutano ya wakuu tu na illi mpate sifa.Thats so bad of you guys kama wana jumuiya mnaowawakilisha watanzania wote.

Anonymous said...

Safi viongozi. Watasema tu. msipofanya kitu watalamimika. Mkifanya kitu watalalamika. Hivi Watz tukoje? Jambo zuri limefanyika.

Anonymous said...

Walichokifanya was really unfair. Ilikuwa Watanzania wote tujulishwe na tufanye like town hall meeting ili tuweze kumuuliza maswali muhimu ya namna anavyoliendesha hilo Bunge la Katiba. Nawashangaa Watanzania pamoja na kuishi Nchi zenye highly freedom of expression and integrity and human rights bado wanaendekeza Bureaucracy ya hali juu.

Anonymous said...

Limefanyika nini Bwana ? msilete mambo ya CCM , tunaambiwa jambo litashughulikiwa huu ni mwaka wa 11 toka watu wametaka huo uraia pacha , miaka yenda hii shehe !!

Anonymous said...

Viongozi wa Jumuiya zetu nawapongeza. Asanteni sana kwa kazi nzuri mnayoifanya.

Anonymous said...

Hata mimi nawapongeza viongozi kutuwakilisha. Suala la uraia pacha ni letu wote. Hata wewe unayelalamika peleka malalamiko yako kwa mbunge wako ili alitetee suala la uraia wa nchi mbili.

Anonymous said...

Mimi nasema hivi, wacheni kulalamika. Malalamiko ya nini? Ujumbe umefika na suala la uraia linasonga mbele. Asante Baba Sitta kwa kuwasikiliza viongozi wetu. Tunaelewa kiongozi hawezi kumpendeza kila kila mtu na hawezi kupendwa na wanajumuiya wote. Kazi wanayoifanya viongozi wetu ni nzuri na Mheshimiwa Sitta fahamu ya kwamba tunawaunga mkono viongozi wetu na wametuwakilisha na tunakushukuru kwa kukutana nao na kwa kuwasikiliza.

Anonymous said...

Jamani na hii imekuwa nongwa? Achaneni majungu. Uraia pacha Oyeee. Tanzania Juuu? Juu Juuu Juuu Zaidi.

Anonymous said...

Bunge la katiba litaanza Agosti 2014. Na ni vizuri tuzidi kulihimiza suala la uraia wa nchi mbili ili lisisahaulike. Wewe namba wani hapo juu na nyinyi mnaolalamika mmeshafanya nini kuendeleza issue yetu hii muhimu kwa wanadiaspora? Sema ulichokifanya, malalamiko tu hayafai na kwa nini usijitambulishe ili tukujue badala ya kuendelea kuwapiga majungu viongozi wenzako kwenye mitandao ya kijamii? Tunakujua ni nani maana jinsi unavyoandika ni kama jinsi unavyoongea. Tumeshakutambua. Wacha majung, fanya kazi! Tanzania Oyee!

Anonymous said...

CCM Oyee! Chadema Oyee! CUF Oyeee! NCCR Oyeee! UKAWA Oyeee! Uraia pacha Oyeee! Hili ni suala letu wanadiaspora. Tuungane pamoja ili kufanikisha changamoto zetu za maisha. One Tanzania, One Diaspora, Two Citizenships!

Anonymous said...

Na tumuunge Mkono Mwakilishi wetu Kadari Singo bungeni ili atuwakilishe vizuri. Siiingo sema, sema usiogope semaaaaa! Katusemeee Singo bungeni na Viongozi wetu msichoke kutusemea. Hawa wanaopinga hawapendi Diaspora na maendeleo yake!

Anonymous said...

Nyinyi bishaneni, mimi na Tanzania yangu tu. Naipenda Tanzania. Nawapenda Watanzania. Mheshimiwa Sitta asante sana baba kwa kukutana na Watanzania na wanadiaspora. Tunakukaribisha Texas ukija tena ili nasi tukuone.

Anonymous said...

Katibu wetu tunakupongeza kwa kazi yako nzuri unayoifanya licha ya hao wanaokuzunguka kuwa na mbwembwe nyingi za kukupaka matope. Na huyo anayekulaumu ni mmojawapo wa wale wanaokuzunguka na kukupaka matope ili uonekane hufai. Lakini kazi yako tunaiona. Mwacheni Katibu wetu afanye kazi yake. Endelea na kazi hao wanaokupiga zengwe ni kama mbwa waoga ambao hufoka kwa kubweka sana na ukiwakaribia utimka mbio. Fanya kazi kijana achana na hao wasiopenda maendeleo.

Anonymous said...

M/kiti Sangiwa endelea kutuwakilisha na sisi wa New England, tushirikishwe. Hongera kwa kazi nzuri.

Anonymous said...

Hata sisi wa California tunakukaribisha Mheshimiwa Sitta. Njoo ututembelee na uone rasmi state anayotokea Mheshimiwa Singo. Na tunakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya Bungeni kwa ajili ya kuleta Katiba mpya na maendeleo ya Watanzania.

Anonymous said...

Huyo aliyelalamika hapo utakuta hata uraia wa Tanzania hana. Hivi wewe ni Mtanzania kweli? Toa identity yako tukujue mbona unaificha?

Anonymous said...

Hivi nani kama Kikwete? Maana baraza lake la mawaziri linachapa kazi sana. Na kama matatizo yapo ni kawaida kwa kila nchi. Huyu Sitta ni kiongozi shupavu na mpenda haki. Tutendee haki baba watoto wetu wapate uraia pacha. Tunatanguliza shukrani zetu kwa Mheshimiwa Rais Kikwete na kwa Mheshimiwa Sitta vile vile kwa kukutana na viongozi wetu.

Anonymous said...

Yaani mimi na Mwanangu amezaliwa huku na wanasema sio Mtanzania. Aka! Upuuzi huu siupendi. Tusaidie spika wa Bunge la Katiba, tuuondoe upuuzi huu Tanzania.

Anonymous said...

Hapa hapapatikani uraia pacha mpaka sisi Wazanzibar tukubali. Tembezeni takrima Zanzibar ili suala lenu lipite.

Anonymous said...

Ha ha ha! Mdau uliyesema wametuahidi muda mrefu lakini hawatekelezi nakuunga mkono kabisa. Ila Bunge lililochaguliwa wanaweza kutusaidia. Sisi inabidi tunyenyekee ili tufanikishe katika hili. Hongera wakuu endeleeni kunyenyekea na kukutana na wakuu ili watusaidie. Kiburi au maneno mengi hayasaidii, ila kukutana na watu muhimu kwenye maamuzi ya suala hili ndio njia pekee itakayofanikisha mipango ya Diaspora. Nasema Viongozi ongezeni kasi na Asanteni kwa kutuwakilisha maana mnatumia muda wenu na sisi hatuwalipi hata senti moja.

Anonymous said...

Badala ya kuwalalamikia viongozi kwenye mitandao, hamuwezi kuwatafuta na kuwakilisha manung'uniko yenu kwa viongozi wenu, uso kwa uso? Kuweni wastaarabu na msichafue hali ya hewa kwenye habari nzuri kama hii bila sababu yeyote.

Anonymous said...

CCM, CCM, CCM

Anonymous said...

Hata mimi Brazil, brazil, brazil maana ni mwendo wa Kombe la dunia. lol!

Anonymous said...

Viongozi msijibishane na yeyote. Chapeni kazi tu. Tumewatuma kuchapa kazi na sio kujibishana na wapuuzi wachache wasiotaka maendeleo. Uraia pacha tunautaka. Tena tuko tayari kwenda Dodoma. Tupeni tarehe na kama nitaweza nitashusha timu Dodoma kuhimiza kama nyinyi mnavyohimiza!

Anonymous said...

Mdau wa Brazil na kombe la dunia hapo juu. Netherlands 5 - Spain 1. Uraia pacha 5 - Wapinzani 1.

Anonymous said...

Huyo mdau wa kwanzaa Ana lake jambo