ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 21, 2011

Anakupenda au anakutumia?

Luquman Maloto

MARAFIKI zangu, wiki mbili zilizopita nilikuwa nachambua mada inayohusu namna tendo la kujichua lilivyo tatizo kubwa kwa watu wengi (hasa vijana).
Ilikuwa mada yenye changamoto nyingi sana.
Nilipokea simu nyingi, watu wakihoji maswali kuhusiana na mada hiyo.
Nakiri kwamba wengi walikuwa na nia ya kuacha, lakini tatizo lilikuwa namna ya kuachana na mchezo huo wenye athari nyingi kisaikolojia na kiafya.
Bila shaka somo lilieleweka vyema.

Baada ya mada hii nitawasaidia rafiki zangu ambao wameathiriwa na tabia hiyo, wameamua kuacha lakini wanasumbuliwa na tatizo la kufurahia tendo la ndoa.
Wapo ambao wamepoteza hamu na wengine wanashindwa kuwafurahisha wenzi wao.
Rafiki zangu, hakuna kama All About Love, hapa utapata kila kitu, baada ya mada hii kufikia ukingoni.
Leo nazungumzia juu ya jambo moja muhimu sana, nitakupa njia rahisi kabisa za kugundua mwanamke mwenye mapenzi ya kweli na yule ambaye yupo kwa ajili ya mambo yake!
Unajua wakati mwingine, unaweza kuwa katika uhusiano na mwanamke ambaye ndani ya nafsi yake hana mapenzi kabisa na wewe, lakini anajifanya anakupenda sana kumbe ana nia  anayoijua.
Wapo wanawake wazuri sana, ambao ukiwa nao kwenye uhusiano unajiona ulivyo mkamilifu na mwenye kujiamini hata mbele ya watu wanaokuzunguka.
Tatizo ni kwenye moyo wake, hana mapenzi, hana nia na wewe, hakuwazii wala hafikirii chochote kuhusu maisha yenu ya baadaye.
Wakati hayo yakiwa akilini mwake, wewe unamhesabia kama mwanamke sahihi kwako, mwanamke wa maisha yako ya baadaye, unayempenda kwa kila hali, lakini hakupendi.
Na kama kweli unampenda kwa dhati ndiyo kabisa huwezi kujua kama hakupendi, kwa sababu wewe utakachokua unajua ni mapenzi tu.
Hata hivyo, si rahisi kuficha kila kitu, zipo tabia ambazo anaweza kuzionesha kwako, lakini kwa kuwa unampenda hutagundua kuwa zinadhihirisha jinsi asivyo na mapenzi na wewe.
Zipo nyingi sana, lakini hapa nitakupa dalili kumi ambazo ukiona mwanamke wako anazo ujue hana penzi la moyoni.

ANAKUTEKA
Mwanamke ana haki ya kudeka kwa mwanaume wake, lakini siyo kwa nia nyingine yoyote zaidi ya kunakshi penzi. Huyu hana nia hiyo, anadeka kwa ajili ya kukupagawisha kimahaba ili aweze kuzishika hisia zako sawasawa.
Mchunguze vizuri, utagundua kwamba hata sauti yake anayoitumia kuzungumza na wewe siyo anayotumia akiwa na shoga zake. Anailegeza kwa kuiremba kwa kila hali.
Anataka kukupagawisha. Hiyo ndiyo nia yake, kukupagawisha sana maana yake hutapindua na hutakuwa na wazo la kuwa na mtu mwingine zaidi yake.

ANAPENDA FEDHA
Ni kawaida mwanamke kumuomba fedha mpenzi wake, lakini huyu asiye na mapenzi ya kweli, huwaza fedha mara zote.
Hata kama utazungumza kuhusu kutoka naye katika matembezi, bado ataulizia kuhusu dau lake.
Ana mahitaji mengi. Mwanamke wa aina hii, ukitoka naye nje ya mji au kulala naye hotelini, asubuhi atataka chake! Jiulize ni mpenzi wako au anajiuza? Mbaya zaidi, hata kama utakuwa mgonjwa na amekuja kukutazama siyo ajabu kabisa kukuomba fedha, akiwa na tabia hii ujue hana mapenzi, anataka kukutumia.

HANA HESHIMA
Kwa kuwa hakupendi na wala hafikirii kuwa na wewe katika ndoa, sifa za uanamke hatakuwa nazo. Inawezekana kabisa anazifahamu vizuri sana sifa hizo, lakini hana muda nazo.
Hasikii ukimwambia kitu, mjeuri na wala haheshimu kauli zako.
Kama mpenzi wako, ambaye una malengo naye ya baadaye, una haki ya kumzuia aina fulani ya mavazi, kampani au tabia ambazo huzipendi.
Kwa mwanamke wa aina hii, kumwambia ni sawa na kumruhusu!  Mwanamke huyu, neno heshima ni msamiati mgumu sana kwake.
Unajua kwa nini? Kwa sababu hakupendi.
Mada bado inaendelea, wiki ijayo tutaendelea, SI YA KUKOSA!
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love na Let’s Talk About Love vilivyopo mitaani.

No comments: