Tunasikitika kutangaza kifo cha Andy Swebe Ambassador mpiga bass mahiri (pichani) kilichotokea leo saa 10 alfajiri Dar Es Salaam katika Hospitali ya Marie Stopes, Sinza baada ya kubanwa na Pumu, marehemu alienda mwenyewe Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa usiku. Msiba upo nyumbani kwake Kijitonyama . Katika uhai wake marehemu amepigia Band nyingi ndani na nje ya Tanzania hususani katika Nchi Dubai, Singapore, Kenya, Uganda na hivi karibuni alikua katika ziara ya kimziki Nchini Marekani akishirikiana na Mwanamuziki Mkongwe, Maestro Kingi Kiki na Maneno Uvuruge. Mazishi yatafanyika Dar Es Salaam siku ya Ijumaa. Marehemu tutamkumbuka kwa tabia yake ya ucheshi na bashasha awapo jukwaani, tunamlilia kipenzi chetu lakini zaidi tumuombee kwa Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele, Marehemu ameacha Mjane.
Andy Swebe (kulia) katika picha ya pamoja na Maneno Uvuruge (kati) na Phanuel Ligate wakati wa ziara yao ya kimziki Nchini Marekani hapa walikua kwenye Baby shower ya Edah Gachuma Columbia,Maryland,
Picha ya pamoja kutoka kushoto Maneno Uvuruge, Andy Swebe, Elius Magembe, Phanuel Ligate, Maestro King Kiki na ma winny Casey
Kulia picha juu na chini ni Andy Swebe akitumbuiza katika Restaurant ya Brentwood iliyopo Mount Rainier, Maryland, wengine ni Maestro King Kiki (kati) na Jojo

Kulia ni Andy Swebe alipokua Boston, Massachusetts

Kutoka kulia ni Maneno Uvuruge, Andy Swebe, Flora Mochiwa na Maestro King Kiki siku Marehemu na wanamuziki wenzake walipowasili Houston, Texas kwa ajili ya show ya Thanksgiving.
Andy Swebe (shoto) akikung'uta Bass kwa umahiri mkubwa wakati wa Thanksgiving, Houston, Texas, kulia ni Jojo.
R.I.P. ANDY SWEBE
1 comment:
Man Lucas,
Taarifa za msiba wa Andy zimenistua na kunihuzunisha sana.
Mwenyezi Mungu Amrehemu Andy kwa amani. Amen.
Fidelis M Tungaraza, Helsinki, Finland.
PS/ Tutafutane kupitia simu namba yangu ni +358405597562
Post a Comment