ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 19, 2011

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, NCCR Mageuzi, Bw. David Kafulila, akiingia ndani ya gari lake, kwa ajili ya kuondoka Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam jana, baada ya kuvuliwa Uanachama.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislam, kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana, wakati akiwahamasisha kuchangia uanzishwaji wa Televisheni ya Kwanza ya Kiislam nchini (TV Iman).
Muuguzi Mkuu wa wa Hospitali ya KCMC Moshi, Bi. Redempta Mamseti, akitoa shukrani kwa Benki ya KCB Tanzania, baada ya kukarabati wodi ya wagonjwa mahututi ‘ICU’. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo tawi la Moshi Bw Rominyika Saitabau.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Jaffarai akitumbuiza kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma mpya ya Kampuni ya simu ya
Airtel ijulikanayo kama Airtel Money, mwishoni mwa wiki Uwanja
wa Sokoine, Mbeya.(picha kwa hisani ya Majira)

No comments: