Dereva wa gari namba T 641 BTL, akimwangalia Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, wakati akiandika maelezo yake, baada ya kukamatwa kwa kuvunja sheria, eneo la Karume, Dar es Salaam jana.
Mwendesha Pikipiki ya abiria (Bodaboda), akiwa amesimama kwenye foleni ya magari, Barabara ya Tanda Mti, Dar es Salaam juzi, huku akisoma gazeti, bila kujali usalama wake.
Mkazi wa jiji (jina halikufahamika) alikutwa na mpigapicha Wetu akihamisha thamani zake kutoka eneo la Kigogo Bondeni. Hata hivyo haikufahamika alikokuwa akizipeleka.
Mchezaji wa kikapu wa Sacramento Kings, Tyreke Evans (katikati) akiambaa na mpira katikati ya wachezaji wa Los Angeles Lakers, Derek Fisher (kushoto) na Kobe Bryant wakati wa robo ya nne ya Ligi Kuu ya mchezo huo Marekani (NBA), iliyochezwa Uwanja wa Sacramento, California juzi.Kings ilishinda kwa pointi 100-91.
Mbunge wa Korogwe Vijijini Bw. Stephen Ngonyani 'Profesa Majimarefu' akiongoza mtumbwi kuvuka mto Ruvu uliojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha milima ya Upare na mto huo kujaa,na kusababisha wananchi wa Majengo na Manga-Mtindiro kukosa mawasiliano. wengine ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw Erasto Sima (katikati) na katibu wa UVCCM mkoa wa Tanga, Bw. Acheni Maulid.
No comments:
Post a Comment