Wanachama na wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF) wakipungia msafara wa Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad baada ya kumaliza mkutano jana jijini Dar es Salaam. Picha na Zacharia Osanga
KATIBU Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad jana alikutana na viongozi na wanachama wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kudhibiti mpasuko ambao umekuwa ukikigawa chama.
Sababu za kukutana nao hazikuwekwa wazi, lakini baadhi ya wachunguzi wa mambo ya Chama hicho walisema ni kutokana na mvutano uliopo baina ya maalumu Seif na mwanachama mkongwe wa chama hicho.
Mpasuko huo unafuatia vurugu na kauli za viongozi kutofautiana hasa baada ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid kutangaza kuwa atagombea nafasi ya Ukatibu Mkuu kupambana na Maalim Seif.
Akisoma risala katika mkutano huo uliofanyika katika Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam, Katibu wa CUF wa Kata ya Manzese ambako kuliibuka vurugu za umwagaji damu baina ya wanachama, Jumanne Ali alisema wanasikitishwa na mgogoro uliotokea ndani ya chama hicho.

Ali alifafanua kwamba mgogoro huo uliotokea ndani ya chama hicho hivi karibuni haungwi mkono na wanachama bali ulifanywa na watu wachache kwa maslahi yao.“ Mheshimiwa Katibu Mkuu sisi wanachama wa CUF tutaendelea kuwa mali ya CUF na tunapenda kuwataarifu wanaotumia Manzese kama sehemu yao kujinufaisha wajue tumewabaini,” alisema.
Alisema kwa sasa watafute kata za kufanyia majaribio ya kutekeleza migogoro yao kwani hawatawavumilia wakiwaona wakifanya mambo kinyume na taratibu za chama.
Akizungumzia mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema wanachama wameshauri mambo mengi ya kukijenga chama ambayo wao kama viongozi watayatekeleza.
Alisema maazimio hayo ni kwamba wanakijenga chama na kwamba mtu atakayekivuruga atachukuliwa hatua kwa kufuata taratibu za chama hicho.
Hivi karibuni, Mbunge wa Wawi kupitia CUF, Hamad Rashid alifika kwenye Kata ya Manzese Dar es Salaam ili kufanya mkutano na wanachama, lakini ghafla watu wanaodaiwa kutoka makao Makuu ya chama hicho walifika Manzese na kufanya vurugu wakimzuia asifanye mkutano.
Tangu hapo kumekuwapo na malumbano baina ya Maalim Seif na Hamad ambaye ametangaza hadharani kwamba atawania nafasi ya Katibu Mkuu wa CUF inayoshikiliwa na Maalim Seif.Nia ya Hamad kuwania nafasi hiyo inaonyesha kumtikisa Maalim Seif ambaye kwa juzi alinukuliwa akisema kama ana ubavu asubiri uchaguzi.

Mwananchi
No comments:
Post a Comment