KWA wiki mbili mfululizo tulikuwa tukijadili jinsi simu na mitandao ya kijamii vinavyowatesa wengi. Tuendelee kuanzia pale tulipoishia wiki iliyopita.
Yeye ni Paulo, amepigiwa simu na Reginald, lakini anaongea kwa mapozi kweli kweli. Chunga unaibiwa, huyo si Reginald, bali ni Regina. Prisca anaongea na Rachel, analegeza sauti, ujue huyo si Rachel ni Richard.
Aidha, katika pointi ya kujiamini, ni vizuri ukawa mkweli, mpenzi wako akikuuliza mtu aliyekupigia simu, usijikanyage kumjibu. Hata kama ni mwanaume, mwambie ili ajue hakuna kitu kibaya.
Wengine huogopa kuwaambia wenzi wao pale wanapopigiwa simu na wapenzi wa zamani na kuishia kuwadanganya. Unatakiwa kufahamu kwamba hilo ni kosa kubwa, maana akigundua, anaweza kudhani mnaendeleza ‘mambo yenu’ au mnataka kukumbushia enzi.
NAMBA YAKO IWEKEE KUFULI!
Siyo kila mtu barabarani anaweza kukuomba namba na ukampa, hiyo ni tabia mbaya. Mpenzi wako hawezi kufurahia unapopigiwa simu kila mara na watu wa jinsi tofauti na yako.
Wewe ni mtoto wa kike, umetongozwa umekataa, lakini unaombwa namba unatoa. Ebo! Sasa ulikuwa unakataa au ulitaka tu kumzungusha?
Kwa watoto wa mjini kumpa namba ya simu, inamaanisha umemkubali. Si mmoja au wawili, wengi siku hizi wananaswa kwa simu tu, yale mambo ya kale ya kwenda kuvizia chini ya mti wa karibu na nyumbani kwao yamepitwa na wakati.

Mtazamo wangu ni huu, mwanamke anayegawa namba yake ya simu hovyo, huyo ni kicheche, kwa sababu anaruhusu mawasiliano ambayo hayatakiwi. Kakukataa, lakini namba amekupa, kesho ukikaza uzi utampata. Huo ndiyo ukweli!
Umempa namba mwenyewe, akikutumia sms ya mapenzi na mwenzi wako akiiona, utamjibu nini? Acha ufisadi wewe!
USIWE MSIRI
Anayekutaka mwambie mpenzi wako, hapo utayafanya maisha yako yawe na amani siku zote. Hauna dhambi, kila baya linalotaka kukupata, unamfahamisha mpenzi wako.
Ni njia nzuri kwa sababu mtu anayekutaka, unaweza usimpe namba, lakini akaitafuta hata kwa watu wa pembeni, kisha akaanza kukusumbua, lakini unapokuwa umeshamwambia mpenzi wako, hiyo ni ngao.
Siku akiona sms mbaya kutoka kwake katika simu yako, ataipuuzia au atakuuliza na ukimjibu, atakuelewa na kuondoa mashaka.
HESHIMU HISIA ZA MWENZAKO
Amekwambia hataki uwasiliane na watu fulani, hebu heshimu anachokwambia, ukifanya vinginevyo au kumzunguka na ‘kusevu’ majina bandia, hapo ni kama unajikaanga kwa mafuta yako mwenyewe.
Kuna siku atajua, halafu amani itatoweka. Anakukataza kuongea na wanaume mara kwa mara, wewe husikii. Hapendi tabia yako ya kupokea simu za wanawake kila saa, unajitia kiburi. Muda si mrefu mtagombana!
Anapowatilia mashaka watu unaowasiliana nao, kisha akakuambia usitishe, kama kweli unampenda, basi acha mara moja! Ukifanya hivyo umeheshimu hisia zake.
KUNA UBAYA KATIKA FACEBOOK?
La hasha! Ni matunda ya kukua kwa utandawazi. Mtanzania asiye na passport, leo anaweza akawa na rafiki Australia ambaye anakuwa anamjuza kila kinachoendelea katika Jiji la Sydney. Hakuna gharama kubwa, anajua yote kwa mtindo wa kuchati kwenye ukurasa wa Facebook.
Mtanzania akiwa nje ya nchi, akitaka kujua muhtasari wa kile kinachoendela nchini kwake, anaweza kutumia gharama nafuu, kuulizia mazingira na usalama wa taifa kupitia ukurasa wa Facebook. Inapeleka watu katika ulimwengu mpya, inazidisha uhalali wa usemi kwamba dunia ya sasa ni kama kijiji kimoja.
Inasaidia kuongeza wigo wa marafiki. Watu wanaweza kubadilishana mawazo ya kijamii, pia wakapeana uzoefu kwa namna mbalimbali. Inawakutanisha watu kwa njia ya kipekee na kuwafanya wazoeane kabla ya kugeuka marafiki wakubwa.
INA ATHARI GANI KIMAPENZI?
Facebook imekuwa ikiwafanya baadhi ya wanaume kuona njia ya mkato kupata wapenzi wa mbali. Akanti yake inajaza marafiki wa kike, hana mpango na wanaume wenzake. Wanakuza wigo wa kunufaika katika ngono.
Msomaji na rafiki yangu, Shadya Ismail aliniandikia ujumbe kwa SMS ambao unasomeka hivi: “Simu ni tatizo lakini huku kwenye Facebook nako ni balaa.
Itaendelea wiki ijayo.
www.glopalpublishers.info
No comments:
Post a Comment