CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Kigoma Vijijini, kimeazimia kuwachukulia hatua kali viongozi na wanachama wake watakaopinga kufukuzwa kwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila katika chama cha NCCR Mageuzi.
Maazimio hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine kimelaani vitendo vilivyofanywa na viongozi wa chama hicho waliofukuzwa mwaka jana.
Kaimu Katibu wa CCM Wilaya Kigoma Vijijini, Mfaume Mkusa alisema kuwa chama kimelaani kitendo cha baadhi ya viongozi waliofukuzwa, kukusanya kadi za CCM na kutangaza kukihama chama hicho wakipinga Kafulila kufukuzwa uanachama wa NCCR-Mageuzi.
Mkusa alimtaja Juma Nzengula ambaye alitambulishwa kwamba ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya CCM kwamba alifukuzwa uanachama wa CCM mwaka
jana kutokana na usaliti alioufanya kwenye uchaguzi mkuu uliopita akiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa Kata ya Nguruka.
Katibu huyo wa Wilaya alisema Nzengula amekuwa akimuunga mkono Kafulila kwa maslahi yake kwa kuwa si mwaachama wa CCM kitu ambacho kwao wanakiona kama vurugu na chama kimewaonya wanachama wake wengine watakaoungana na mwanachama huyo aliyefukuzwa.
“Kamati ya siasa inalaani kwa nguvu zote yeyote aliyekusanya kadi za CCM kupinga kufukuzwa kwa Kafulila, hao sio wanachama hivyo waondolewe kwenye chama kwa mujibu wa katiba ya CCM.
No comments:
Post a Comment