NI matumaini yangu kwamba umzima, bukheri wa afya na uko tayari kukisoma kile ambacho nimekuandalia kwa siku ya leo.
Wiki hii nitazungumzia mbinu za kumuacha mpenzi wako bila kumuumiza. Katika ulimwengu wa mapenzi, kila siku watu wanaingia kwenye uhusiano lakini elewa kwamba siku ambayo wewe unamzimikia mtu flani siku hiyo hiyo wapo wanaozinguana na kuachana.
Si kwa wapenzi tu, hata kwenye ndoa wapo ambao leo hii ndiyo wanaoana lakini leo hii hii kuna wanaopeana talaka. Iko hivyo na kwa maana hiyo suala la kupendana lipo lakini la kuachana nalo halikwepeki.
Ndiyo maana ukijaribu kufuatilia hata wewe unayesoma makala haya yawezekana mpaka umefikia hatua uliyonayo umeshaacha au kuachwa.
Hilo ndilo limenifanya niandike mada hii. Je, unajua mbinu sahihi za kumuacha mtu ambaye mlikuwa mkiambiana I love you, I love you too? Kama jibu ni hapana, leo nitakupa shule inayoweza kukuongoza katika hilo.
Lakini kabla ya kulizungumzia hilo niseme tu kwamba miongoni mwa vitu nisivyovipenda katika maisha yangu ni kusikia flani na flani waliokuwa wanapendana sana hadi kuwa gumzo mtaani wameachana.

Inaniuma kwa sababu najua ivavyouma. Mara nyingi anayeachwa anaumia zaidi hasa akiwa hajajiandaa na ndiyo maana wataalamu wa masuala ya mapenzi wamejaribu kuanisha mbinu ambazo unaweza kuzitumia katika zoezi zima la kumuacha mpenzi au mume/mke wako hasa pale zinapokuwepo sababu za msingi zinazoweza kukubalika.
1. Hakikisha umedhamiria
Unatakiwa uwe umejiandaa kumkosa katika maisha yako. Jadiliana na akili pamoja na moyo wako kama kweli vimeridhika na uamuzi unaotaka kuchukua. Jiulize ni kweli amekukosea kiasi kwamba huwezi kuendelea kuwa naye?
2. Usiwe mwenye hasira
Unapotaka kumuacha mpenzi, mume au mke wako kwa sababu maalum, hakikisha huna hasira.Tulia ili hata pale utakapokuwa hauko naye usije ukajuta na kudhani hukuchukua uamuzi sahihi.
3. Muda na siku sahihi
Wataalamu wa mapenzi wanasema kuwa, muda wa asubuhi siyo mzuri kumuacha mpenzi wako kwani utampa wakati mgumu siku nzima lakini pia kwa wapenzi wanaofanya kazi siku za katikati ya wiki siyo siku nzuri.
Siku ya Ijumaa jioni inapendekezwa kuwa siku nzuri ya kumuacha mpenzi wako kwa maelezo kwamba ataitumia wikiendi kujiliwaza na hata inapofika Jumatatu, anakuwa amepoa tayari kwa kuendelea na majukumu yake.
Wiki ijayo tutaendelea kuona njia sahihi unazoweza kuzitumia katika kumuacha mtu uliyetokea kumpenda ambaye huenda ulimuahidi kwamba hutamuacha, usikose.
No comments:
Post a Comment