Salum Maige, Sengerema
MTOTO Mariam Charles (8), ameuawa kikatili kwa kupigwa na fimbo na dada yake baada ya kusahau kununua dawa aliyoagizwa dukani.Mwenyekiti wa mtaa, Elikana Kitula, alisema tukio hilo lilitokea saa 4:00 usiku wa kuamkia juzi Kitongoji cha Sekondari Road, Kata ya Ibisabageni, wilayani Sengerema, mkoani Mwanza.Mariam anadaiwa kufikwa na mauti hayo kutokana na kipigo kutoka kwa dada yake aliyekuwa akiishi naye kwa lengo la kulea mtoto wake.
Mama mwenye nyumba alikopanga mtuhumiwa, Elizabert Laurent (82), alisema mtoto huyo alipigwa na dada yake kwa kutumia fimbo kubwa na wakati akitenda ukatili huo alikuwa amemfungia kwenye chumba cha kupikia.

Laurent alisema chanzo ni pale mtoto huyo aliposahau kununua dawa aina ya Action aliyoagizwa dukani, ambako alinunua Panandol hivyo alipoipeleka nyumbani dada yake alipata hasira na kumfungia ndani kisha kumfanyia ukatili huo.
Hata hivyo, licha ya maumivu aliyopata mtoto huyo kutokana na kipigo hicho, aliagizwa tena na dada yake kufuata dawa hiyo, hali iliyosababisha kuondoka moja kwa moja kwenda mitaani kujificha kwa kuhofia maisha yake, hadi alipookotwa na wasamaria wema na kumrudisha nyumbani.
Mashuhuda wa tukio hilo, walisema wakati akirudishwa nyumbani baada ya kuokotwa eneo la Mahakama ya Mwanzo Ibisabageni, alikuwa akitokwa na damu sehemu za kifuani huku akiwa na jeraha kwenye paji lake la uso.
Waliongeza kuwa mtoto huyo ilipofika jioni bila huruma, dada yake alianza tena kumpiga hadi kuzirai na saa 3:00 usiku hali yake ilibadilika kutokana na maumivu aliyopata, saa moja baadaye alifariki dunia.
Waliendelea kudai kuwa mtoto huyo amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili vya kupigwa na dada yake, licha kuonywa na majirani zake.Pia, inadaiwa vitendo hivyo viliwahi kuripotiwa kwa viongozi wa mtaa na Mtendaji wa Kata ya Ibisabageni, Japhet Mashara, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na viongozi hao kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Polisi wilayani Sengerema walifika eneo la tukio na kumchukua mtuhumiwa, huku mume wake akitoroka baada ya tukio hilo.Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali Teule Wilaya ya Sengerema, ukisubiri kusafirishwa kwenda nyumbani kwao kisiwani Kome kwa mazishi.
Mwananchi
2 comments:
akae jela milelel huyu dada mi binafsi kabla ya kumaliza kusoma hii yote nilishikwa na uchungu sana kama namjua huyu dada....
tatizo kubwa la africa ni wanaamini adhabu ni kupiga tu sio kuongea na kuangalia tatizo liko wapi.
RIP little girl
mwenyezi mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi. Sijui wazazi wao wamejisikia vipi masikini!
Post a Comment