ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 25, 2012

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja Atia Saini Mikataba Mitatu Ya Utafiti Wa Mafuta Nchini


Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akiwekeana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Motherland Industries Limited kutoka India Bw, V. K. Sood (Kulia) uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta nchini, umefanyika leo jijini Dar es Salaam,

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akiweka saini mkataba wa utafiti wa mafuta nchini kwa kampuni tatu kutoka nje, (kushoto) ni Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Bw, Yona Killagane na (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Matherland industries LTD kutoka India, Bw. V.K. Sood .(kulia). Mkataba huo umewekwa saini leo kwenye jingo la Wizara ya Nishati na Madini
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akifafanua jambo wakati wa uwekaji saini wa mikataba mitatu ya uatafiti wa mafuta kutoka kampuni za nje jijini leo DSM (Kulia) ni Kamishna Msaidizi wa Nishati (Petroleum na Gas ) Bw, Prosper Victus
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) akibadilisha hati za makubaliano ya utafiti wa mafuta nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda (kulia) , hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Slaam wakati wa hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa kampuni kutoka nje
Kamishna Msaidizi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw, Prosper Victus (alisimama mbele na Kabrasha) akitoa maelezo ya awali wakati wa uwekaji wa saini mikataba mitatu ya utafii wa mafuta kutoka kampuni za nje leo wakati wa hafla hiyo kwenye jengo la Wizara ya hiyo jijiji Dar es Salaam.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

Picha kwa hisani ya Haki Ngowi

No comments: