Fabio Capello leo ametangaza kujiuzulu kuifundisha timu ya Taifa ya Uingereza baada ya mkutano wake na viongozi wa chama cha mpira wa miguu cha Uingereza.
Wachunguzi wa mambo wanasema uamuzi Fabio Capello wa kujiuzulu ni kutokana na shinikizo toka chama cha mpira wa miguu cha Uingereza cha kumshinikiza kumvua Unahodha mchezaji John Terry, ambapo yeye aliwashauri wasubili maamuzi ya mahakama kwanza lakini chama cha mpira wa miguu cha Uingereza kilikataa ushauri huo.
Mapema leo Fabio Capello alikutana na Mwenyeki wa FA, David Bernstein na katibu mkuu wa chama hicho, Alex Horne kwenye ofisi za FA zilizopo Wembley kuzungumzia swala hilo lakini kutokana na FA kubaki na msimamo wao wa kumvua unahodha wa timu ya Taifa mchezaji John Terry ndiko kulikopelekea kwa Fabio Capello kuamua kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo ya Taifa ya Uingereza.
Chama cha Mpira wa Miguu cha Uingereza kimeukubali uamuzi wa Capello kujiuzulu na kusema huo ni uamuzi muafaka na kimemtakia kila la heri kule aendako.
No comments:
Post a Comment