Saturday, February 25, 2012

HAFLA YA KUMUAGA SEFUE YAENDELEA KWENYE UBALOZI WA TANZANIA , NEW YORK

 
Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiongea machache kuwashukuru Watanzania waliotoka sehemu mbali mbali kuja New York kwenye Halfa ya kumuaga iliyofanywa kwa kushirikiana kati ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani na Ubalozi wa kudumu waTanzania Umoja wa Mataifa, New York iliyofanyika Ijumaa Feb 24, 2012 katika Hotel ya Millenium UN Plaza na baadae kuhamia kwenye Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar akiongea machache kumshukuru na kumpongeza Balozi Sefue kwa kusema yeye angependelea kutumia jina la Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Balozi kwa sababu Katibu Mkuu Kiongozi yupo peke yake, Balozi wapo wengi na anapokwenda kushika wadhifa wake mpya anaomba asisahau ugaibuni na siku zote atakua mfano wa kuigwa.

Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Dr. Asha Migiro nae akiongea machache kwenye Hafla ya kumuaga Mhe. Balozi Sefue.

Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York, akiongea machache na kumtakia Mhe. Sefue kila la heri kwenye kazi yake mpya na siku zote atakumbukwa na WanaNew York kwa kuleta Umoja na mshikamano kwenye Jumuiya yao.

Mwenyekiti wa mamrekebisho ya katiba DMV kwa niaba ya Watanzania Metro Politan Area akiongea machache kumpongeza Mhe. Sefue.

Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania, Houston, Texas nae akiongea machache kumpongeza Mhe. Sefue na kumtakia kila la heri.

Kiongozi wa Watanzania Chicago, IL akiongea machache na kumpongeza Mhe. Sefue kwa Wadhifa wake mpya pia aliwakaribisha Watanzania wote Chicago kwenye sherehe za DICOTA ambazo mwaka huu zitafanyikia huko kwenye wiki ya Labor Day Weekend.

Viongozi wa DICOTA nao wakiongea machache na kumtakia Mhe. Sefue kila la heri na kamwe hawtamsahau kwani bila yeye DICOTA isingefikia hapa ilipo.

Kiongozi wa Watanzania, North Carolina akiongea machache na kumuasa Mhe. Sefue kwamba Serikali isiwasahau Watanzania waliopo Nje wanaweza kuchangia maendeleo nyumbani na kuleta mabadiliko makubwa pindi watakapopewa nafasi ya kufanya hivyo.

Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania California nao wakiongea machache kumpongeza Mhe. Sefue.

Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania Massachusetts nae akimpongeza Mhe. Sefue.

Kutoka kushoto ni Biabusha, Afisa Ubalozi Dr. Mkama, Mhe. Balozi Maajar na Mhe. Balozi Sefue wakipiga picha ya pamoja kwenye sherehe za kumuaga zilizofanyikia kwenye Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York.

Kutoka kushoto ni Kaimu Balozi, Mhe. Lilian Munanka, Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Dr. Asha Migiro na Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar.

Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kulia) akiongea jambo na na mwambata wetu wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, Brigedia Jenerali Maganga.

Mhe. Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawili matatu na Dr. Crispin Semakula.

Kwa picha zaidi Bofya Read More

4 comments:

  1. viongozi wote wa watanzania ktk state wanaume, jamani kina dada inakuaje?

    ReplyDelete
  2. Wabongo twapenda sherehe.

    ReplyDelete
  3. tuko busy tunasoma tukimaliza utatuona

    ReplyDelete
  4. Tuko busy na schedule siunajua wanaume wengi hawana kazi za kueleweka kwa hiyo Kama hizo zinawafaa ili angalau waweze kukuza majina Yao wao wanadai(kumentaine status)

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake