NAAM, kiafya mimi ni mzima, sijui wewe mwenzangu, naimani u mzima wa afya, kama ni mgonjwa basi nakupa pole kisha namuomba Mungu akupe afya njema. Baada ya hayo, turejee kwenye mada yetu ya leo:
Nina imani uliyemchagua kuwa mpenzi wako ni chaguo la moyo wako, hasa nikizingatia kuna wanawake wengi au wanaume wengi lakini upo na huyo uliyenaye.
Inawezekana uliyenaye si wewe wa kwanza kumpenda, huenda yeye alikupenda kabla yako, ila akashindwa kukuanza kutokana na uzito wa mdomo wake au desturi ya mila zetu kuwa mmoja ndiye mwenye uwezo wa kuongea lile linalomsibu juu ya matamanio ya moyo na mwili.
Kwanza lazima tujue kukaa pamoja au kuchagua mpenzi ni bahati nasibu, unaweza ukapenda kiasi cha kufa na kuoza lakini mwenzako yupoyupo hajali mateso ya moyo wako, anachojali ni kuufurahisha mwili wake na siyo kufurahisha nafsi ya mpenziwe ambayo ndiyo inayotaabika.
Nina imani kila atafutaye mpenzi, hutafuta wa kufa na kuzikana, wapo wanaoanza uchumba mpaka ndoa kamili, pia wapo wanaowataka watu kwa ajili ya kuangalia mwanamke ana nini kutokana na sura yake, umbile lake au sauti ambayo hujiuliza akiwa hivi sauti yake ipo hivyo, je, kwenye shughuli inakuwaje?
Mwingine anavutiwa na utanashati wako au pengine ‘u-handsome’ au hata umbile lako la kimazoezi ndivyo vinavyomfanya ajisikie kufanya mapenzi na wewe lakini siyo kwamba anakupenda.
Wapo wanaofuata fedha zako na pale zinapoisha na mapenzi pia huisha. Wapo wanawake duniani wasiojua dunia inakwenda wapi na nini hatima ya maisha yao, hawa wanakutana na wanaume baa na kulala nyumba ya wageni na baada ya hapo hamjuani.
Lakini wapo ambao wana mapenzi ya dhati waliojitoa kimwili na kiakili, siku zote huwa na maswali magumu mioyoni mwao na kuwafanya waishi kwa mashaka kwa kuhofia kukupoteza.
Kama nilivyosema kuchagua mpenzi ni bahati nasibu, hakuna aliye mjuzi wa kuchagua mpenzi aliye safi, inategemea karata uliyofunua. Kama utapata karata nzuri hapo mshukuru Mungu kwa kukupatia mpenzi mzuri mwenye haruma na mapenzi ya kweli.
Nina imani ndani ya mapenzi umpendaye siku zote huumia moyoni na kujiuliza maswali haya ambayo ni wewe wa kuyajibu.
Kwa kupitia kona hii, unatakiwa kuyajibu kwa vitendo kwa kuwa wengi wamekuwa na mapenzi ya mdomoni.
Ni maswali yapi na unapaswa kumjibu vipi? Tukutane wiki ijayo.
www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment