Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
TUMSHUKURU Mungu kwa kuendelea kutupendelea na kutupa afya njema siku ya leo, hakika yeye ni muweza wa yote na tuendelee kumuabudu.
Ngugu zangu, leo napenda nizungumzie mchakato wa katiba mpya ya nchi, suala ambalo lilitikisa bunge wiki iliyopita.
Nimeguswa sana na jinsi Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete anavyosimamia vyema mchakato wa kuwapatia Watanzania katiba mpya safi.
Ngugu zangu, leo napenda nizungumzie mchakato wa katiba mpya ya nchi, suala ambalo lilitikisa bunge wiki iliyopita.
Nimeguswa sana na jinsi Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete anavyosimamia vyema mchakato wa kuwapatia Watanzania katiba mpya safi.
Nakumbuka mwaka jana wakati mchakato huo ulipoanzishwa, wakosoaji wengi walisema walikuwa na mashaka kama kweli Rais Kikwete alikuwa na nia ya dhati alipotangaza kwamba angehakikisha nchi yetu inakuwa na Katiba mpya ifikapo mwaka 2014 na kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Wasiwasi wa wakosoaji hao bila shaka ulitokana na utamaduni uliozoeleka katika nchi nyingi za Afrika, ikiwamo Tanzania ambapo maamuzi mengi yanayofanywa na viongozi wa serikali hizo aghalabu hufanyika kisiasa kwa lengo la kuvinufaisha vyama vilivyopo madarakani, huku wakijitahidi kuvidhoofisha vyama vya upinzani.
Naamini hata hapa Tanzania kuna baadhi ya viongozi wa chama tawala wana mawazo hayo lakini Rais Kikwete amekuwa kinyume. Nampongeza sana!
Hakuna ubishi, wananchi wengi hasa wanachama wa vyama vya upinzani awali waliamini kwamba Rais Kikwete kwa vyovyote vile asingesimamia upatikanaji wa Katiba mpya itakayopatikana kwa maridhiano na mwafaka wa kitaifa.
Nikiri kuwa Rais Kikwete amewashangaza watu wengi, wakiwamo wabunge na wanachama na wafuasi wa chama chake cha CCM, kwa msimamo wake wa kutaka ipatikane katiba mwafaka iliyoridhiwa na wananchi wote.
Wengi tunajua kuwa Rais Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, lakini baadhi ya wananchi wakasema wazi kuwa ulipitishwa kishabiki bungeni kwa wingi wa wabunge wa chama chake cha CCM.
Wahenga walisema,’serikali ina mkono mrefu’, naamini Rais Kikwete alisikia tetesi hizo za kupitishwa kishabiki sheria ile, hivyo akaamua kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani Ikulu na kukubaliana nao mawazo kuhusu baadhi ya vipengele katika sheria hiyo ambavyo vinahitaji kufanyiwa marekebisho kwa masilahi ya taifa.
Wiki iliyopita kuliwa na tetesi kutoka bungeni kuwa wabunge wa CCM walitishia kuukataa muswada huo kwa madai kwamba marekebisho ya sheria hiyo yangekiweka chama chao kitanzini na kukipa Chadema nguvu kubwa ya kisiasa.
Pengine ni vyema kukumbuka kuwa, Chadema ilisusia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba mwaka jana baada ya kuona hoja zao kuhusu muswada huo zilikuwa zinapuuzwa na wabunge wa chama tawala kwa kutumia wingi wao.
Kitendo cha Rais Kikwete kukutana nao Ikulu na kusikiliza na kukubali hoja zao, hata baada ya kusaini muswada huo kuwa sheria, inadaiwa ndicho hasa kilichoibua hasira za baadhi ya wanachama na wabunge wa CCM.
Ikadaiwa kuwa baadhi ya wabunge waliamua kususia kujadili muswada huo na kukataa ombi la Rais aliyetaka kukutana nao mjini Dodoma hivyo kulazimisha wakae kama kamati mara kadhaa ili kuwashawishi wasisuse.
Tunaambiwa baada ya majadiliano waliunda timu ya wajumbe watano ili wakutane na Rais Kikwete kama mwenyekiti wa chama hicho. Wajumbe hao walikutana naye, ingawa ni mapema mno kujua kiongozi huyo wa nchi alitumia mkakati gani kulainisha msimamo mkali wa wabunge hao, kiasi cha kukubali kuujadili na kuupitisha muswada huo.
Lakini kiukweli naamini kwamba Rais Kikwete alikubali hoja za Chadema kwa sababu aliona siyo tu zilikuwa zinaboresha sheria hiyo, bali pia zilikuwa zinazingatia masilahi ya taifa.
Niwakumbushe watu wote kwamba tunapojadili katiba mpya ya nchi tusiangalie itikadi za chama, kila mmoja aweke akilini na apime madhara ya kuyakataa marekebisho ambayo yana faida na manufaa kwa taifa kwa kuangalia upande mmoja wa shilingi, yaani chama.
Ndugu zangu, naamini siyo vema kama leo nitaorodhesha yale yote ambayo asasi na vyama mbalimbali vya siasa vilivyomuona rais na kutoa mapendekezo ambayo yalikubaliwa na kiongozi wa nchi na kuingizwa katika muswada wa marekebisho ya sheria hiyo.
Lakini nichukue nafasi hii kumpongeza Rais Kikwete kwa kusimama kidete kulinda masilahi na umoja wa taifa letu pasipo kutetereka ama kuyumbishwa na siasa za itikadi za vyama kwa sababu hili ni jambo zito sana.
Nimpongeze pia kwa kutambua kwamba Katiba ya nchi ndiyo sheria mama ambayo ni dira inayoongoza shughuli za mamlaka zote, ikiwamo mihimili mitatu ya dola ambayo ni bunge, mahakama na serikali kuu, katiba hiyo itakuwa halali pale tu wananchi wote watakaposhirikishwa katika mchakato wote wa kuipata na akitokea mtu au kundi kutaka iandikwe kwa masilahi yao, basi hao si wenzetu na wapigwe vita kali kabisa.
Niwashukuru wabunge wote waliojadili marekebisho yake kwa kutetea masilahi ya nchi kwa sababu naamini wamefanya vile kwa ajili ya ustawi wa taifa letu leo na vizazi vijavyo.
Ni dhahiri wale wote waliokuwa wakiweka mbele kipaumbele chao au chama chao au kundi fulani katika mjadala wa mchakato huu wa kuelekea kwenye katiba mpya ya nchi, watakuwa wameonekana na naamini Mungu pia kawaona, sasa atawafanya nini, mwenyewe anajua.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment