Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akimnadi mgombea ubunge wa tiketi ya CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi huo kwenye Uwanja wa mpira wa Ngaresero
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru
Mashariki kwa kishindo, kwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuhutubia mamia ya wakazi wa mji
mdogo wa Usa River ambao ni kitovu cha jimbo hilo akiwaomba wamchague mgombea wa CCM, Siyoi Sumari.
Uzinduzi huo wa kampeni za CCM, jana ulibadili hali ya kisiasa Usa River kutokana na Chadema
kuonekana kuhodhi mji huo kwa siku kadhaa tangu walipozindua kampeni kwa mgombea wao
Joshua Nassari, Jumamosi.
Mashariki kwa kishindo, kwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuhutubia mamia ya wakazi wa mji
mdogo wa Usa River ambao ni kitovu cha jimbo hilo akiwaomba wamchague mgombea wa CCM, Siyoi Sumari.
Uzinduzi huo wa kampeni za CCM, jana ulibadili hali ya kisiasa Usa River kutokana na Chadema
kuonekana kuhodhi mji huo kwa siku kadhaa tangu walipozindua kampeni kwa mgombea wao
Joshua Nassari, Jumamosi.
Mkapa, ambaye jana alipanda jukwaani katika uwanja wa michezo wa Ngaresero akiwa na
kaulimbiu ya ‘Naweka Mambo Sawa’, alitumia mkutano huo kupuuza hoja mbalimbali zilizotolewa na Chadema, akisema anafanya hivyo ili kuweka mambo sawa.
Akihutubia wanaCCM hao, Mkapa alishangazwa na uzushi kwamba alikipa masharti chama
hicho kilipomtaka kuzindua kampeni hizo, akisema waliotoa uzushi huo ni waongo, wazushi na watu waliokosa adabu.
“Walisema nikija Arumeru nitazomewa… nataka kuweka mambo sawa, je, nimezomewa sijazomewa?” Alihoji Mkapa na kujibiwa na umati wa watu ‘“Hujazomewa”.
Alisema badala ya kuzomewa kama ilivyodaiwa na wapinzani, alipokewa kwa chereko na nderemo.
“Nataka kuweka mambo sawa… walisema nimetoa masharti kwa CCM ili nije nizindue kampeni
Arumeru. Huu ni uzushi wa kijinga sana na waliosema hivi hawana adabu kabisa. Kwanza
hawakuniuliza mimi, wasaidizi wangu na wala hawakufika ofisini kwangu.
“Mimi ni zao la CCM. Siwezi kumwekea masharti Mwenyekiti wangu ambaye ni Rais wangu pia,
nimekuwa Rais na Mwenyekiti wa Chama Taifa siwezi kumkosea adabu Mwenyekiti na Rais wa sasa (Jakaya Kikwete). Lakini pia siwezi kuiwekea masharti wala kuikosea adabu CCM, Kamati
Kuu, Halmashauri Kuu wala viongozi wangu wa CCM.”
Pamoja na kupuuza hoja hiyo alisema imelenga kupotosha ukweli, na kupuuza uzushi kwamba
ana mashamba aliyopora kwa wananchi katika Jimbo la Arumeru na kuwapa wazungu walowezi.
Alikanusha huku akibeza wapinzani waliodai kwamba angezomewa. “Katika maisha yangu sijawahi kumnyanyasa mwananchi yeyote Arumeru, Arusha wala Tanzania nzima katika suala la ardhi.
Wanasema nina ubia na singasinga na Mholanzi gani sijui wanaomiliki mashamba hapa. Katika maisha yangu nitatumia nguvu zangu na uwezo wangu wote kuhakikisha kuwa Mtanzania hanyanyasiki kwa kudhulumiwa ardhi,” alisema.
Alitumia nafasi hiyo kuipuuza Chadema kwamba ni chama kisicho na sera na kinachotumia kaulimbiu ya Peoples' Power (Nguvu ya umma) kama sera katika kurubuni wananchi jambo alilosema ni la hatari.
“Wanasema tu Peoples' power lakini neno hilo ndio linaeleza wataleta vipi maji? Watakusanya
vipi mapato ya Serikali? Watawajengea vipi barabara? Na wataboreshaje huduma nyingine muhimu kama CCM wanavyoeleza?” Alihoji Mkapa.
Alieleza pia kushangazwa na mtindo wa Chadema kupinga kila jambo bila kutoa suluhisho na
akashangazwa na hatua ya baadhi yao kutumia jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kama mtaji wa kisiasa.
“Kuna mmoja anasema eti yeye ni mtoto wa Nyerere. Nimekaa na Mwalimu Nyerere kwa miaka 25 nikiwa katika nafasi mbalimbali kuanzia Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Serikali, Mwandishi wa Habari wa Rais na Waziri wa nafasi mbalimbali sikuwahi kumsikia wala kutambulishwa huyo mtu… mambo ya ajabu sana haya,” alisema Mkapa.
Alisema CCM ina uhakika wa kushinda uchaguzi huo kwa vile mgombea wake, Sioi Sumari ni mtu makini, mpole, mwenye huruma na akili za hali ya juu katika kuona jimbo hilo linasonga mbele kimaendeleo.
Akihutubia kwenye mkutano huo, Sumari alisema atafanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele
muhimu vitatu vya uboreshaji wa huduma za maji, ajira kwa vijana, ujasiriamali na uboreshaji wa miundombinu ya barabara.
Mapema, Mweka Hazina wa CCM Taifa, Mwigulu Nchemba alipuuza hoja kwamba kwa CCM
kumteua Siyoi kugombea ubunge kuziba nafasi ya baba yake, marehemu Jeremiah Sumari ni sawa na kuleta utawala wa kifalme akisema ni hoja isiyo na msingi.
“Chadema wanasema hivyo lakini hebu angalia Ndesamburo (Mbunge wa Moshi Mjini), mtoto
wake ni Mbunge na mwali wake pia ni Mbunge (hakuwataja). Dk Slaa (Willibrod Katibu Mkuu), mkewe ni Mbunge, Tundu Lissu ana mdogo wake ni wabunge, Vincent Nyerere … Leticia Nyerere wote ni wabunge… sasa ni vipi wanatusema, Siyoi ambaye tena baba yake alishafariki
dunia,” akisema Nchemba.
Habari Leo
No comments:
Post a Comment