Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ludewa, Mkoa mpya wa Njombe, kimepata pigo baada ya Diwani wake wa Kata ya Mlangali, Rudolph Chaula, kukatisha maisha yake baada ya kuamua kujinyonga akiwa ndani ya ofisi yake akidaiwa kufanya hivyo kwa lengo la kukwepa madeni.
Marehemu Chaula kabla ya kufikwa na mauti hayo, alikuwa ni Meneja wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Mlangali (Saccos).
Taarifa za kuaminika zilizopatikana na kutoka wilayani humo zinaeleza kuwa diwani huyo alijinyonga usiku wa kuamkia juzi akiwanyumbani kwake, Mlangali.
Vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kuwa marehemu Chaula pia alikutwa ameacha ujumbe wa maandishi uliogubikwa na utata.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa chanzo cha diwani huyo kujinyonga, ni kuzidiwa na mzigo wa madeni kutoka Mlangali Saccos.
Mmoja kati ya wanachama wa Mlangali Saccos ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini alisema yeye si msemaji wa chama hicho, lakini anachokifahamu ni kwamba katika siku mbili zilizopita, alitembelewa na wakaguzi ambao walifanya ukaguzi katika chama hicho cha ushirika na kubaini kuwapo deni kubwa lisilojulikana mkopaji.
“Mheshimiwa diwani wetu ambaye alikuwa ni mhasibu (meneja kwa sasa) katika Saccos hiyo. Kabla ya wakaguzi hao alikuwa ni mchangamfu kupita kiasi. Ila baada ya wakaguzi kuja, alionekana ni mtu mwenye msongo mkubwa wa mawazo. Jambo hilo liliwafanya wananchi wengi kuingia na shaka juu ya usalama wa fedha zao,” alisema.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Mlangali Saccos ilikuwa ni moja kati ya vyama vya ushirika vyenye nguvu kubwa wilayani humo ila baada ya mhasibu wao huyo kuingia katika siasa na kugombea udiwani mwaka 2010 ndipo chama kilipoanza kuyumba.
Chanzo hicho kilisema kutokana na kutoonekana kutwa nzima usiku ndipo walipomkuta akiwa amejinyonga kwa kamba katika chumba chake ambacho alikuwa akitumia kama ofisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, amethibitisha kwa njia ya simu kutokea kwa tukio hilo na kwamba mara baada ya kupata taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo taarifa rasmi itatolewa kwa umma.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake