Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar (kushoto) akipiga picha ya pamoja na mwimbaji wa nyimbo za injili Flora Mbasha alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani uliopo Washington, DC.
Ijumaa, March 23, 2012
Mwimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini Tanzania, Flora Mbasha atembelea Ubalozi wa Tanzania katikati ya jiji la Washington DC, Marekani. Mtumishi huyu wa Mungu kupitia muziki wa injili alipata nafasi kuwa mgeni rasmi wa Mh. balozi
Mwanaidi Sinare Maajar siku hiyo, ambapo Mhe, balozi huyo alizungumzia fursa mbalimbali zipatikanazo nchini Marekani na Tanzania. Aidha Flora Mbasha alimwagia sifa Mhe, balozi kwa mafanikio makubwa ya kuwaunganisha watanzania walioko huku ughaibuni. Pamoja na hayo Flora Mbasha alimshukuru Mheshimiwa balozi kwa kazi yake nzuri hapa nchini Marekani. Zaidi ya hayo Flora alitoa shukrani za kipekee kwa watanzania waishio nchini Marekanina kwa ukarimu wao, upendo na mshikamano miongoni mwao.Mwisho Flora alitoa shukrani za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya M. Kikwete kwa kuweza kuendeleza amani na mshikamano nchini Tanzania. Habari hii imeletwa kenu na Alex Kassuwi, kutoka Washington DC, USA. Kwa mawasiliano kuhusu flora kwa wale waishio US wapige namba 301 305 9685, pia unaweza ukampata kwenye skype na facebook
Mbashas
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC wakiwa na Mwanamuziki Maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania Flora Mbasha.
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC wakiwa na Mwanamuziki Maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania Flora Mbasha.
Kutoka kushoto, Emmanuel Mbasha, Ms. Maganga, Flora Mbasha, Mindi kasiga na Alex Kassuwi
Picha juu na chini ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mbasha akifanya mahojiano na watangazaji wa VOA Mary Mgawe (Mrs Malinda) kushoto na Sunday Shomari (kati)
Flora Mbasha Alipohojiwa na Voice of America
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzanaia, Flora Mbasha (kushoto) akiwa kwenye ofisi za VOA na Dr. Hamza Mwamoyo.Picha juu na chini ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mbasha akifanya mahojiano na watangazaji wa VOA Mary Mgawe (Mrs Malinda) kushoto na Sunday Shomari (kati)
No comments:
Post a Comment