![]() |
| Kikosi cha SE Setif’ ya Algeria. |
KOCHA Mkuu wa timu ya ES Entente Sportive Sétifienne ‘SE Setif’ ya Algeria, Alain Geiger amesema mchezo wao na Simba Jumapili katika michuano ya Kombe la Shirikisho utakuwa mgumu kuliko walivyotarajia.
Hatua hiyo inatokana na uzoefu wa Simba katika michuano ya kimataifa, hali ambayo inawapa hofu kubwa.
Akizungumza jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kocha huyo alisema wamejiandaa vilivyo kwa mchezo huo, lakini wanajua Simba si timu ya masihara.
Hatua hiyo inatokana na uzoefu wa Simba katika michuano ya kimataifa, hali ambayo inawapa hofu kubwa.
Akizungumza jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kocha huyo alisema wamejiandaa vilivyo kwa mchezo huo, lakini wanajua Simba si timu ya masihara.
Mashabiki mbalimbali wa soka jana walijitokeza kwenye mazoezi ya timu hiyo, huku kocha huyo akisema kwa sasa wanafanya mazoezi mara moja tu ambayo ni asubuhi.
Geiger, mlinzi wa zamani wa kimataifa wa Uswisi, alisema wanazo taarifa nyingi kuhusiana na Simba ikiwemo kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek mwaka 2003 jijini Cairo, Misri.
Kocha huyo ambaye alikuwa akizungumza kwa lugha ya kifaransa huku akitafsiriwa na nahodha wa timu hiyo, Mourad Delhoum, alisema rekodi ya Simba katika michuano ya kimataifa wanaiheshimu.
Kikosi cha Setif kina wachezaji watatu wa kulipwa ambao ni kiungo Sofiene Zaaboub ambaye ni raia wa Ufaransa, Valentin ambaye ni raia wa Burkina Faso na mshambuliaji Cyrille Ndaney raia wa Cameroon. Wachezaji wengine wote waliosalia ni Waalgeria.
Kuelekea mchezo huo timu hizo zimekuwa zikitambiana kila moja kwa nyakati tofauti kuwa zitaibuka na ushindi katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho.
Leo makocha wa timu hizo mbili, Mserbia Milovan Cirkovic wa Simba na Geiger wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo huo.

No comments:
Post a Comment