Advertisements

Thursday, March 22, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI PAWAGA

Rais Jakaya Kikwete akifungua maji ya bomba kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika kijiji cha Itunundu kata ya Pawaga Iringa uliogharimiwa na kanisa la Anglican Dayosisi ya Luaha Mkoani Iringa kwa zaidi shilingi bilioni mbili, Huku wakuu wa kanisal hilo wakishuhudia, kutoka kulia ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Luaha Dornald Mtetemela, Martha Mgomi Mratibu wa mradi huo na Askofu Joseph Mgomi wa Daayosisi ya Luaha. FULLSHANGWE ilikuwepo katika msafara huo na kukuletea taswira mbalimbali za kuwasili kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete pamoja na shughuli yake ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Itunundu kata ya Pawaga mkoani Iringa.
Rais Jakaya Kikwete akimpongeza mama Agnes Msavi mara baada ya kumtwisha ndoo ya maji kuashiria ukombozi kwa mwanamke kutokana na kukamilika kwa mradi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakilipoti tukio hilo huko Pawaga Itunundu.
Rais Jakaya Kikwete akiwasili kijijini Itunundu Pawaga tayari kwa kuzindua mradi huo.
Vijana wa Kimasai wakicheza ngoa yao wakati wakimkaribisha Rais jakaya Kikwete kijijini hapo leo.
Warembo wa kimasia wakiwmlaki Rais Jakaya kikwete huku wakiwa wameshikilia bendera za taifa alipowasili katika kijiji cha Itunundu.
Umati wa wananchi ukimsubiri Rais Jakaya Kikwete katika kijiji cha Itunundu.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamanda wa vijana mkoani Iringa Salim "Sas" Abri mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kada wa Chama cha Mapinduzi Venance Mwamoto.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Askofu wa Dayosisi ya Luaha Joseph Mgomi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mjini Iringa leo mchana, kushoto ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Luaha Dornald Mtetemela.
Rais Jakaya Kikwete akiwatunza wasanii wa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati alipowasili mjini Iringa leo.
Kwa picha zaidi Bofya Read More
Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma kushoto mara baada ya kuwasili mjini Iringa leo, kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Grayson Rwenge.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamanda wa polisi mkoa wa IringaEvarist Mangalla katika uwanja wa ndege wa Nduli.
Rais Jakaya Kikwete akipungia wananchi mkono mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli mkoani Iringa leo mchana.
Ndege iliyomleta Rais Jakaya Kikwete ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Nduli leo mchana.

No comments: