Tuesday, March 6, 2012

Wakina Mama Mkoani Mbeya waanza Kuazimisha siku yao ya Wanawake Duniani kwa kupanda miti katika Milima ya Shule ya Sekondari Isyesye

Baadhi ya wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya wakichukua miti tayari kwenda kupanda kwenye milima ya Isyesye.
Mwanasheria wa Mkoa wa Mbeya wa kwanza kutoka kushoto  akiongozana na Afisa habari pamoja na Afisa Biashara kwenda kupanda miti katika Milima ya Isyesye.
Wakina mama wengine wakiwa wanapandisha Mrimani kwa Furaha kwenda kupanda Miti.

Wakina Mama wakiwa wamejipanga Tayari kwa kuanza kupanda Miti .
Wakina mama wakiwa wanapeana ushauri jinsi ya kuweka mti katika shimo ili wapate upanda Vizuri
Mama akiwa katika mpango mzima wa kuchimba Mashimo kabla ya kupanda miti
Mwanasheria wa Mkoa akiwa anapanda Mti katika Milima ya Isyesye 
Afisa Habari wa Mkoa wa Mbeya akiwa anapanda mti katika Milima ya Isyesye Leo
Wanaume nao walikuwepo wakiwasindikiza akina Mama kupanda Miti katika Milima ya Isyesye
Kwa picha zaidi Bofya Read More
 Afisa Habari wa Mkoa wa Mbeya akiwa bega kwa bega na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Isyesye  katika kupanda miti 
 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Isyesye  aikwa pamoja na wakina mama wakishirikiana kupanda Miti
Hili ni eneo la Nje kidogo na sehemu ambapo wakina mama walikuwa wanapanda miti, Kulikuwa na Mihogo ya Kupunguzia Njaa.
Picha zote na mwandishi wetu Maalum  Joseph mwaisango ambae yupo kwenye eneo la tukio Muda Huu.

Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu

1 comment:

  1. Hilo ni jambo la la mbolea kwa utunzaji wa mazingira na kuweka mandhari ya shule hiyo kuwa ya kuvutia. Ikiwezekana akina mama nchini kwetu kote wangeiga tabia hiyo kokote walipo. Siyo kina mama peke yao hata kina baba, vijana na wanafunzi wangeweza kuwaunga mkono pia.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake