Ahmed Hossam “Mido” akiifungia Zamalek bao la ushindi.
Michael Momburi, Cairo
YANGA imepanga kukata rufaa kwa Shirikisho la Soka Afrika CAF kwa madai kuwa mchezo wao dhidi ya Zamalek ulikuwa na mazingira mengi ya utata juzi kwenye Uwanja wa Jeshi la Misri.
Mabingwa hao wa Tanzania walifungwa bao 1-0 baada ya Mido kuunganisha krosi ndefu kutoka kushoto na Yanga kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu walitoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya awali Mjini Dar es Salaam.
YANGA imepanga kukata rufaa kwa Shirikisho la Soka Afrika CAF kwa madai kuwa mchezo wao dhidi ya Zamalek ulikuwa na mazingira mengi ya utata juzi kwenye Uwanja wa Jeshi la Misri.
Mabingwa hao wa Tanzania walifungwa bao 1-0 baada ya Mido kuunganisha krosi ndefu kutoka kushoto na Yanga kuondoshwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu walitoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya awali Mjini Dar es Salaam.
Tangu juzi usiku viongozi wa Yanga walikuwa na vikao vya mara kwa mara huku Mwenyekiti na wajumbe wote wakijenga hoja ili kuwasilisha rufaa hiyo sambamba na vielelezo.
Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema wanafikiria kukataa rufaa kutokana na maamuzi ya utata, mashabiki kuingia uwanjani pamoja na kucheza katika mazingira ya presha.
"Kwanza lile bao halikuwa goli, yule mfungaji alikuwa ameotea kabisa vielelezo vipo na video inaonyesha, waamuzi wa pembeni walikuwa hawapandishi vibendera kuonyesha wenzetu wameotea mpaka kipa wetu anapodaka mpira, halafu tumecheza kwenye mazingira ya kijeshi ambayo yaliwapa presha wachezaji wetu,"alisema Nchunga.
Alisema,"halafu kingine walisema watakuwa na watendaji 30 tu, lakini uwanjani walikuja watu wengi tu ambao ni kinyume na utaratibu kwa timu iliyofungiwa na walikuwa wanashangilia,"alisema Nchunga.
Lakini hadi jana mchana Yanga walikuwa hawajawasilisha rufaa hiyo ingawa wanachama matajiri waliokuwa jijini hapa wakiongozwa na Seif Ahmed waliweka fedha hiyo ya rufani mezani ambayo ni dola 1500.
Wanachama hao walikuwa wamewaahidi wachezaji jumla ya sh. 2 milioni kila mmoja endapo wangeifunga Zamalek juzi Jumamosi.
KIIZA
Mshambuliaji Hamis Kiiza amechukizwa baada ya kukabiliwa na maumivu makali ya dakika za mwisho ambayo yalimkosesha mechi ya juzi dhidi ya Zamalek jijini hapa.
Kiiza aliumia kwenye mazoezi ya Alhamisi usiku na kuikosa mechi hiyo muhimu ambayo Yanga ilifungwa bao 1-0 na Zamalek kwenye Uwanja wa Jeshi jijini Cairo.
"Nilikuwa naamini kwamba ningecheza, lakini imeshindikana naumwa sana, yaani hizi mbavu zinaniuma sana nilitonesha kidogo usiku Alhamisi na ukichanganya na hii baridi ya hapa ndio balaa kabisa,"alisema Kiiza.
"Nilitaka sana kucheza huo mchezo, haya maumivu yalianza tangu Tanzania, lakini nikajua yataisha sasa imekuwa tatizo, lakini ngoja nipate matibabu tuone nini kitatokea,"alisema Kiiza ambaye alifunga bao la Dar es Salaam Yanga ilipotoka sare ya bao 1-1 na Zamalek kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment