
Elizabeth Michael (Lulu)
MSANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi
kuwa kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.
Habari zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa, Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumza na simu
kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake.
"Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo
Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na kuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari wa Kanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali.
"Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha Polisi Oysterbay kuchukua PF3," kilisema chanzo hicho.
Chanzo kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu asiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi.
Katika hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada ya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba, walioandamana wakidai wanamtaka Lulu.
"Tunataka jembe letu", waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokea Barabara ya Ali Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askari waliokuwapo kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaa kutuliza ghasia kama zingezuka.
Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa,
Msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili jana kuwa Lulu atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mara baada ya polisi kupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa Serikali.
“Tunasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu kubaini chanzo cha kifo hicho kwa sababu wamechukua baadhi ya sampuli za marehemu kwenda kupima na kwamba tutakabidhiwa leo(jana). Kimsingi tukipata tu taarifa hiyo tutamfikisha mahakamani,” alisema Kenyela.
Aliongeza ripoti hiyo itaweza kuwasaidia kuandika mashtaka ili yaweze kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.
Kamanda Kenyela alisema kuwa, ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwamba imeonyesha kuwa Kanumba amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.
Msanii Stephen Kanumba alifariki usiku wa Ijumaa Kuu.
Mwananchi
12 comments:
mimi ninafikiri kwa usalama wa LULU inabidi akae sehemu ya usalama zaidi maana watu wnahasira cna kwa hivyo anaweza kupata kipigo kutoka kwa watu wenye hasira kali,au kuuawa na wananchi au kundi wa watu kwa hivyo basi tunaomba awekwe pahali pa usalama,ili haki itendeke na sheria ichukue mkondo wake.
Lulu anaweza kufa kwa mambo mengi mfano usongo wa mawazo , kupigwa na watu wenye hasira kali au kuwekewe sumu endapo atakuwa uraiani ,au kurogwa hadi kufa ...... kwa ufupi Lulu maisha hayana safari ndefu ....
Bado ni mdogo huyu dada ndio maana alikimbilia "coco beach" lakini bado kafanya kosa kubwa yaani hapo maisha yake yote watamwonyeshea kidole heri aje ulaya aanze upya na aachane na mambo ya umaarufu kwa mana hauna mpango...... manake kama akifungwa akitoka ni mzee na hakuna anaemkumbuka tena kutoka itakuwa shida sana kwa huyu dada na yeye hana wasiwasi wa kukaa jela sababu hajui bado kuwa hapo ndio kafika akitoka polisi ni kwenda keko na kuwa huru baada ya miaka kadhaa. aweke loya mzuri.
pole sana lulu
jamani lulu
pole sana manake huchi ni kilio kingine sijui hata wazazi wake huyu lulu wana hali gani manake kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuua kwa umri huo ni mbaya sana.
lets not judge her for now.
Tuombe haki itendeke..kwasababu bado hatujui ukweli kwamba uyo binti aliusika kwa namna moja au nyingine katika kifo cha kanumba..nina mashaka na uamuzi ambao mahakama yetu itauchukua bila kujali uchunguzi wa kina unafanyika...nafkri haitakuwa haki kumtia binti hatiani pasipo uchunguzi wa kina kufanyika na kubaini kama binti yuko hatiani au ni kitu kingine ndo kilisababisha icho kifo...nashangaa amekimbilia kumkamata bila hata ya uchunguzi wa kina kumamilika ...kumbukeni daktari wa Michael jackson walimtia atiani baadaya ya uchunguzi kubaini kwamba alisababisha kifo cha staa huyo.....Inasikitisha Tanzania haki iko wapi.
Tuache kulia bila ya kutaka haki kutendeka huo utakuwa unafiki....mimi mwenyewe nimeguswa na kifo cha kanumba lakini ningependa kuona Haki inatendekea.
Mdau dresen-Germany(mwanaharakati).
A Person is innocent until proven guilty but in Tanzania a person is gultly unless you prove innocent later . It is sad let give this young girl the benefits of law first. pole Lulu next time date somebody your age.
kweli unavyosema lakini ni heri akae huko huko aktoka tu watamuua watu wanaompenda kanumba manake mpaka ionekane hana kosa ni afanye kazi aache kazi....
pole sana dada lulu nakushauri uache mambo ya uselebriti
huyu dada hajui anashtakiwa kwa nini? ni umri tu namwonea huruma sababu akija kushtuka miaka kadhaa imeshapita hajui kuwa watu huwa wanakukimbia saa una matatizo hata kama wewe ni so called celebrity
Hivi mnajua marehemu Kanumba mara yake ya mwisho aliyofanya physical check up?
siajabu alikuwa ni mfu anayetembea....wewe unaye muhukumu Lulu uanajua Health status yako?Na hili liwe nifundisho kwa mijibaba inayofanya ngono na watoto under age na kuwaharibia maisha yao.
Bi shamba wa DC.
kweli mkuu umeongea maneno ya busara kabisa na mamlaka husika inabidi iyazingatie!
Yawezekena kabisa Kanumba alikuwa na issue nyingine ya kiafya ambayo kwa sasa watu wanaona ni aibu kuitoa hadaharani. Kwani mtoto wa miaka 17 wa kike kumsukuma baba wa miaka 28 kuna kitu kilichotokea, aidha Kanumba alikuwa anampiga huyu mtoto. Watu maarufu hufa kwa sababu mbalimbali na tusisahau kuwa na wao ni binadamu. Uchunguzi ufanyike wa kisayansi (forensic). Na kama alianguka wakati anamkimbiza lulu who knows? Sijasema Lulu ni malaika but uchunguzi wa kina ufanyike, siyo kwa sababu mwingine ni maarufu kuliko mwingine.
bi wa shamba ushauri wako ni upi? tuwe tunafanya physical check up kila siku au? na nani aliyekuambia Lulu alikuwa under age, huyu binti alifanya mzinga wa part to celebrate her 18th birthday, as far as i know huwezi kupata licence ya ku endesha/to own a car Tanzania if you are under 18. Fundisho should be kwa hao under age pia
Post a Comment