ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 26, 2012

ATCL hewani tena Mei

Mwandishi Wetu
NDEGE za Shirika la Ndege la Tanzania (ACTL) zinatarajiwa kuruka tena kabla ya mwishoni mwa mwezi ujao na zitafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na miji ya Mwanza na Kilimanjaro.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa ATCL, Paul Chizi, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa tovuti ya shirika hilo.

Alisema kwa sasa shirika linawasubiri maofisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)) ili waende Misri kukagua ndege itakayochukuliwa na shirika hilo kwa ajili ya safari za ndani ya nchini na kwamba hatua huyo itafutiwa na ya kupata ndege zingine mbili.

Kuhusu ndege inayotengenezwa katika karakana ya shirika hilo, DASH- 8 alisema inatarajiwa kuwa tayari ndani ya wiki sita au nane.

Alisema ATCL itaendelea kuzingatia umuhimu wa kutoa huduma bora ili kukidhi matarajio ya wateja wake .

“Watu wanaulizia kuhusu lini tutaanza safari zetu, nawahakikishia kuwa tunajipanga vizuri ili tuwahudumie vizuri tena ndani ya muda mfupi ujao,” alisema Chizi.

Kuhusu tovuti  alisema itasaidia kuwasiliana na wateja na kwamba itakuwa na taarifa zote zinazohusu shirika hilo.

Alisema kuzinduliwa kwa tovuti hiyo ni hatua muhimu katika ufanisi wa kazi za shirika.
Alisema kupitia tovuti hiyo ya  www.airtanzania.co.tz wateja watakuwa katika nafasi nzuri ya kushughulikia safari za ndege za shirika hilo hata wakiwa nje ya nchi.

“Lakini pia kupitia mitandao ya jamii kama facebook na twitter ambayo shirika limejiunga nayo , wateja na wananchi kwa jumla watapata fursa ya kutoa maoni yao kuhusu njia bora za kuendelea kuboresha shirika hilo na kuuliza maswali,” alisema Kaimu mkurugenzi.

1 comment:

Anonymous said...

AIr tanzania is one of the sad stories about privatization of state owned corporations in tanzania, for those who still remember how air tanzania was, before being privatized they will agree with me that, its performance in terms of how it was managed and customers service provision was poor. but the fact that, the company had 4 aircraft of its own and 1 aircraft which was leased from abroad is the evidence that things were not so bad at that time compared to the current situation cause air tanzania does not own a single aircraft at the time being, of those4 aircraft i have mentioned above all of them were bought brand new in 1978 from seattle washington state by the late julius nyerere government . its inconceivable that after privatization of air tanzania in early 2000`s all of the aircraft were sold and replaced by 2 leased aircraft by the so called "investor" from south africa...smell fishy enhe? in addition to that air tanzania had assets like houses in and outside tanzania worthy millions of dollars,,,, what happened to these houses? don't ask me .. you know exactly what went down after privatization , mafisadi bought all these houses by give away prices, the truth is that air tanzania will not be able to dig out of its grave. it is gone for good. RIP air tanzania. the solution is not investors but better management by patriotic tanzanians themselves.