Chadema, Dk. Willibrod Slaa kutokana na kauli zake za uchochezi alizotoa kwenye mkutano wa hadhara mwishoni mwa wikiiliyopita katika Viwanja vya Sahara mjini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Philipo Kalangi, alisema kauli za Dk. Slaa ni za uchochezi ambazo
zinaweza kuharibu amani ya nchi.
Mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano wa hadhara, Dk. Slaa alitoa wiki moja kwa Polisi mkoani hapa kukamata waliohusika na vurugu katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kirumba Aprili mosi.
Vurugu hizo ambazo zinadaiwa kufanywa na wafuasi wa CCM, zilisababisha kujeruhiwa kwa
wabunge wa Chadema, Samson Kiwia wa Ilemela na Salvatory Machemli wa Ukerewe.
Katika mkutano huo, Dk. Slaa alisema iwapo Polisi haitawakamata watuhumiwa na kuwachukulia hatua za kisheria ndani ya siku saba, yeye atachukua jukumu
la kuhamasisha wananchi wa mkoa huu kuwakamata vijana hao.
Kamanda Kalangi alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na hivyo kauli za Katibu Mkuu huyo haziwezi kulilazimisha
Jeshi lake kufanya kazi kwa matakwa yake.
“Ofisi yangu inafanya kazi bila kushurutishwa, na mpaka sasa watu 18 wamekamatwa na kuhojiwa kuhusu tukio hilo ila kuna baadhi ya watu ambao wako nje kwa dhamana kutokana na kukosekana maelezo ya kujitosheleza,” alisema Kamanda Kalangi.
Kalangi alisema polisi hawawezi kushikilia watu ambao hawana maelezo yoyote, kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza na kuandikisha maelezo ambayo
yatawaweka hatiani watuhumiwa hao.
Wabunge hao walishambuliwa usiku wa manane
na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando
kabla ya kusafirishwa hadi Hospitali Kuu ya
Muhimbili, Dar es Salaam ambako walilazwa pia kwa
matibabu zaidi na wamesharuhusiwa.
Kutoka Dodoma Sifa Lubasi anaripoti, kwamba
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Pudenciana
Kikwembe (44), kutoka Mkoa wa Katavi, amevamiwa
na kuporwa fedha na kadi tatu za benki wakati akiwa
kwenye baa ya Lady May barabara ya Iringa mjini
humo.
Akisimulia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen, alisema kuwa
tukio hilo lilitokea saa 8.30 usiku wa kuamkia jana
kwenye baa hiyo.
Alisema mtu asiyefahamika, alivamia baa hiyo
akiwa na gobori na kumpiga risasi ya mguu mkaanga
chipsi, Ally Kubula (22).
Alisema baada ya kumjeruhi mkaanga chipsi huyo
ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Dodoma akitibiwa majeraha, alipora mikoba miwili;
mmoja ukiwa wa Mbunge huyo wenye dola 600 za
Marekani, Sh 180,000 na kadi za benki za NMB,
CRDB na NBC.
Pia alipora mkoba mwingine wa Sharon Tuli, rafiki
wa Mbunge huyo, ukiwa na simu mbili na Sh
100,000.
Kamanda alisema juhudi za kumsaka mtu huyo
zinaendelea na Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi
kupitia sera ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi, kutoa
taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuhakikisha wanabainika
na kuchukuliwa hatua stahiki.
Kupitia mtandao wa kompyuta, Mbunge huyo
alikiri kuporwa fedha na kadi za benki.
“Ni kweli kwamba tukio hilo lilitokea jana (juzi)
saa 2.30 usiku katika baa ya Lady May Pub, iliyoko
barabara ya Iringa … nilifika mahali hapo kupata
chakula na kuzungumza na wanafunzi wa vyuo
vikuu na taasisi za elimu ya juu zilizoko Dodoma
wanaotoka Rukwa na Katavi kuhusu mambo mbalimbali,”
alisema Mbunge.
Alitaja miongoni mwa mambo hayo ni hatima ya
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye anatoka
Katavi.
“Wanafunzi hawa walikuwa na shauku ya kujua
hatima hiyo kutokana na mambo yalivyokuwa yamejitokeza
ndani ya Bunge. Nimependa kuweka hili
wazi ili kuiwezesha jamii kufahamu yaliyojiri na pia
kueleza ukweli, kwani wapo baadhi ya watu ambao
wameanza kutafsiri tukio hili kwa namna tofauti kwa
sababu wanazozijua,” aliongeza.
Sambamba na hilo, wanafunzi hao walikutana na
Mbunge huyo kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo
katika mikoa ya Rukwa na Katavi na suala la
ajira na mambo yanayowahusu kimasomo.
Kamanda Zelothe alisema Jeshi la Polisi linatoa
mwito kwa wamiliki wa baa, kufuata sheria, kanuni
na taratibu zinazoelekeza namna ya kufanya biashara
zao, ikiwamo kufunga kwa wakati, ili kuepusha
vitendo vya uhalifu.
Habari Leo
No comments:
Post a Comment