ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 18, 2012

HII NDIO EMAIL YA IDDI SANDALY KWA TAMCO

From: iddi sandaly <mbezi@yahoo.com>
To: Islamic Chama <tamcotuwasiliane@yahoogroups.com>
Sent: Tuesday, April 3, 2012 11:06 PM
Subject: TAARIFA RASMI ZA UCHAGUZI WA DMV

Ndugu zangu wana TAMCO,
Napenda kuwajulisha rasmi kwamba mimi ndugu yenu Iddi Seif Sandaly kuwa nagombea nafasi ya Kuwa Mwenyekiti wa jumuia ya watanzania DMV. Kama
wengi wenu mnavyonifahamu ni kwamba tumeshirikiana wote katika mambo mbali mbali  na mnanijuwa kiundani kabisa ni jinsi gani nilivyo na pia mnazifahamu sifa zangu za uongozi.
 
Lengo langu ni kuwa kiongozi ambaye nitatetea masilahi ya Watanzania wote waishio hapa DMV. Kama tujuavyo jumuia yetu ya watanzania hapa DMV imekuwa ikikumbwa na viongozi wasio madhubuti na wenye kuleta makundi. Nadhani ni muda sasa kwa watu makini kukifufua na kukiimarisha chombo hichi cha DMV.
 
NAOMBA KURA YAKO.
 
 
Uchaguzi utafanyika siku ya Jumapili; Tarehe 15, April 2012. 
 
Muda 2.00PM
 
Mahala; Mirage Hall, 1401 University Blvd, Hyattsville, MD 20783
 
 
Nakuomba USIKOSE NA wajulishe wengine
Wenu

5 comments:

Anonymous said...

Toa messages nyingine ambazo ulituma juu ya Loveness kuwa siyo mwenzetu, pia elimu...ki ukweli Iddi ulipiga kampeni mbaya sana ya udini tena mbaya sana, mimi ni muislamu mwenzako lakini sipindi kuwagawa watu hasa kwa dini.

Anonymous said...

Sasa je huu ni udini?au ni ule usemi wa kizungu unisema "charity start at home" kwa mtazamo wangu nadha sio vibaya mtu kumwambi mpenzi wake umependeza sana. Kwa watanzania tuwe wakweli na tuacheni majungu na fitna. Wahenga walisema 'FITNA'haijengi ila huishia kwa 'FITNA'tupendane Kama rangi ya bendera yetu. Blue,nyeusi,njano na kijani zote ni rangi za matumaini. Mungu ibariki tanzani. Mungu ibariki Africa. Mdau Washington

Anonymous said...

What is he trying to accomplish? Why don't we move forward since time for politics is over.

Anonymous said...

mdau hapo juu toa evidence. hupendi kuwagawa watu, lakini ulichoandika hapo ndio sumu mbaya zaidi. uchaguzi umekwisha sasa tusonge mbele kuleta maendeleo ya jumuiya yetu hii azimu.

Anonymous said...

Mpwa funga malumbano ya kura. Focus na ya mbeleni. We gladly like to hear new ideas kwa maendeleo. All these dramas are turn off kwa watz wengi. Y dont you all drop these dramas please kuweni wastaarabu.