Advertisements

Friday, April 13, 2012

IDDI SANDALY FOR PRESIDENT


Iddi Sandaly ni Kaka yenu , Mdogo wenu, rafiki yenu na ni mwenzenu.
Nimekuwa nikijumuika nanyi katika mambo mbalimbali ya kijamii, kwenye furaha na uzuni.
Pia nimekuwa ni kijifunza mengi tu kwa kushirikiana na watu wote wa hapa DMV na walio nje ya DMV.
Sina Kashfa hapa DMV na wala sijawahi kuwakashifu watu wengine, Sibagui mtu, nacheka na kuongea na kila mtu bila kujali kama wewe umetoka Musoma au Mafia.

Malengo yangu kama mtanipata nafasi ya kuwa Raisi wa Jumuia ni:

  1. Kuimarisha Umoja wa Watanzania hapa DMV
  2. Kurudisha imani na Umaninifu kwenye jumuia hii.
  3. Kutatua matatizo ya wana DMV hapa DMV- Home first.
  4. Kuanzisha Business Chambers za Wana DMV
  5. Kuwa na Kamati ya michezo hapa DMV
  6. Kuhakikisha haki za wana DMV zinalindwa.
  7. Kuhakikisha kuwa Serikali yetu ya Tanzania inatutambua na kuutambua mchango wetu katika nchi.

Naomba kura Zenu
Iddi Sandaly

6 comments:

Anonymous said...

Hatuna jinsi wewe Unasifa na Rafiki wa kila mtu.

Anonymous said...

Jembe mpini...DMV imepata mipini miwili...Iddi + Cherehani = Jembes

Anonymous said...

bwana Idd wewe ni kaka yetu tunakupenda, ila umefanya kosa moja kutumia udini kujipatia kura. Omba samahani kwa hilo kwani Watanzania wote ni ndugu bila kuangalia itikadi za kidini, kabila na siasa.

Anonymous said...

Wewe Anonymous 09.19 ; usilete siasa za CCM hapa. Hebu tupe ushahidi kwamba Iddi katumia udini. Usianze siasa zenu hapa. Jamaa huyu Iddi ni mtu safi sana. Wacheni hizo.

Anonymous said...

Wewe anony wa 02.08 una makengeza aliesema ni wa saa 10.37am sio 09.19.kwanza huyo cherehani mwenyewe mdini na mambo yake ya kanisani tu hata msibani hawamjui wapeni watu wanaojichanganya na jumuiya na wanaojua shida za watu mitaani sio cherehani hajui kitu hajui mutu,haendi sehemu,fikirieni mtakuja juta.

Anonymous said...

Combination ya Iddy + Cherehani = Minimum Education level Masters plus CPAs.
Combination ya Love + Kinyemi = MAXIMUM ASSOCIATE DEGREE.
Bora kuongozwa na kina ZAYUMBA au JOHN KISOMO ? Mimi nachagua walifuta ujinga kwani kwa sasa ni viongozi sehemu zao za kazi.Cherehani ni accountant wa ubalozi wa AU zamani "OAU" hapa USA.Iddy ni mhasibu alibobea mpaka wengine hawataki kusikiliza interview yake hapa vijimambo.DMV we deserve better.