ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 2, 2012

KAMANDA GULUMO WA MSONDO NGOMA AREJEA JUKWAANI KWA KISHINDO BAADA YA KUPONA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA

Wasanii wa bendi ya Msondo ngoma wakitoa burudani katika viwanja vya Sigara Dar es salaam jana kushoto ni Shabani Dede na Muhidini Gulumo ambaye amerudi kwa kishindo baada ya kuwa benchi kwa wiki mbili wakati akiwa anaumwa na sasa yupo fiti kuendelea kutoa burudani kwa wapenzi wa bendi hiyo Jumapili April 1, 2012 walimalizia wiki End katika ukumbi wa Max bar Ilala Bungoni.Msemaji wa bendi ya Msondo Ngoma RAjabu Mhamila SUPER D kulia akicheza sambamba na wapenzi waliojitokeza katika bonanza hilo.
Waimbaji wa bendi ya msondo ngoma wakiwajibika wakati wa onesho lao lililofanyika katika viwanja vya klabu ya sigara Dar es salaam jana kushoto ni Eddo Sanga na Shabani Dede bendi hiyo Jumapili April 1, 2012 ilikua katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni
Msemaji wa bendi ya Msondo ngoma Rajabu Mhamila SUPER D akicheza wakati wa bendi hiyo ikitumbuiza.
Wadau wa msondo ngoma ambao ni Waandishi wa habari wakijadiliana jambo wakati wa burudani hizo jana kushoto ni Tulo Chambo na Juma Kasesa

No comments: