TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Katika kuhakikisha kuwa timu ya taifa ya ngumi inapata maandalizi
mazuri kabla ya kwenda kushiriki mashindano ya kufuzu kuelekea
Olimpiki .leo kuanzia saa 4.00 asubuhi kumefanyika mashindano timu ya
taifa na timu ya ngumi ya jkt.matokeo ni kama ifuatavyo;-
1-49kg l/fly said hofu wa jkt amemshinda john christian taifa kwa majaji 3,0
2.52kg fly abdalah kassim taifa amemshinda amdani issa wa jkt kwa majaji 2,0
3. 56kg bantam emilian patrick taifa amemshinda revocatus chomari wa
jkt kwa majaji 2,0
4. 60kg l/weight elias damson jkt amemshinda Denis maritn wa taifa kwa
majaji 2,0
5.64kg l/welter victor njaiti wa taifa amemshinda kassimu hussein wa
jkt kwa dakitari
kusimamisha pambano baada ya kassim kuchanika juu ya jicho
6. 69kg welter selemani kidunda wa taifa alimshinda gurudani saidi wa
jkt kwa k.o round
ya kwanza
7. 91kg heavy weight kati ya ditram kaimbe wa jkt na haruna swanga wa
timu ya taifa pambano ambalo lililokuwa na mvuto na msisimko
mtangazaji alishindwa kutangaza matokeo baada ya kuzongwa na mashabiki
wa pande zote kutaka mchezaji wao atangazwe mshindi.hadi tunaondoka
timu ya taifa bado itakuwa na jaribio moja na kombaini ya vyombo vya
ulinzi na usalama kabla ya kwenda morocco.
kwa sasa timu ya taifa ipo kambini mkuza kibaha katika shule ya
filbert bayi chini ya makocha watatu na daktari mmoja
timu hiyo ina tarajiwa kuondoka tarehe 26/04/2012 kuelekea morocco
kushiriki mashindano ya kufuzu kushiriki olimpiki julai london
uingereza
hadi kufikia leo tumepata jumla ya tiketi sita kutoka kamati ya
olimpiki tanzania toc.
ambazo ni kwa ajili ya wachezaji 4na makocha2. hata hivyo bft bado
inaomba wafadhiri kwa ajili ya kuongeza idadi ya wachezaji na viongozi
wa bft kwa ajili ya kuhudhuria kikao muhimu cha shirikisho la ngumi la
afrika.
taarifa hii imeletwa na makore mashaga katibu BFT,mara tu baada ya
kumalizika kwa mashindano hayo. 0713588818
No comments:
Post a Comment