ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 16, 2012

MPWA NAE APIGA KURA DMV

Mpwa nikipiga kura kwenye uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Mirage uliopo Langley Park, tunamshukuru Mungu uchaguzi ulikuwa wa haki na amani, Mungu Ibariki Jumuiya yetu, Mungu wabariki viongozi wetu, uwape hekima, uwatie nguvu, umoja na mshikamano, Wanajumuiya tuwe kitu kimoja tuwape ushirikiano Viongozi wetu. Mungu ibariki DMV, Asante

Mapaparazi wakifuatilia uchaguzi kutoka kushoto ni Iska Jojo, Swahili Villa, Tito Mazali na Mr. Omar

Wasimamizi ya masanduku ya kupigia kura.
Mama Safari akitumbukiza kura yake
Mzee Safari akitumbukiza kura yake.
 Benja Mwaipaja akitumbakiza kura yake
Watanzania wa DMV wakiwa kwenye mkutano
 Fay na Geradin wakipata picha ya pamoja
 Kutoka kushoto ni Omby, Jack na Catherine wakiwa kwenye mkutano wa uchaguzi.
 Omby na Catherine wakipata picha ya pamoja.
 Cholo (kushoto) na Al- Amin wakipata ukodak moment.
Dullah (kushoto) wakipata picha ya pamoja ni Kilemile
 Nyasu na Cesil wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Picha ni Nyasu 

7 comments:

Anonymous said...

huyo dada mwenye blue dress mrembo sana!!

Anonymous said...

wewee Ligei kubwa(mpwa)ulipigia Loveness,baada ya matokeo ulinywea sanaaaaaa.

Anonymous said...

Hivi wabongo mbona hamna ustaarabu!!huyu Mpwa anakuleteeni habari,anaunganisha wabongo wote na ana haki ya kumchagua yeyote mbona alikua anaweka habari za wagombea wote bila ubaguzi,leo hii mnamtukana???nakuona umekaa kwenye kompyuta yako unainjoi Vijimambo lakini unamtukana huyu Mpwa wa watu,kushindwa kwa Loveness sio jambo la ajabu ndungu,na kwa taarifa yako Loveness ni mshindi in anyhow!!!wala Luka hakunywea ndio kwanza mnazidi kuwapa nguvu watu wote waliokua Team Loveness.Hii ni kazi ya kujitolea,tuone hao waliochaguliwa wasije jutia.Mtafakari kabla hamjaongea badilikeni wajamaa!>

Anonymous said...

Mimi ni mkazi wa DMV kwa muda wa zaidi ya miaka 16!nina familia yangu hapa na mkazi wa hapa kwa miaka yote niliyoishi!kwanza nawapongeza watanzania wote waliokuja kwenye huu uchaguzi ambao haujawahi kujaza umati wa watu kama huu!bila malumbano wala ugonvi!hiyo ni credit kubwa.Vilevile wagombea wa viti hivyo hasa waliogombea uwenyekiti naona hao ndio ilikuwa tageti kubwa sana,nampongeza Idi na Loveness lakini pongezi nyingi zinakwenda kwa Loveness!huyu mama ni shupavu na tunataka wanawake kama yeye kwenye jumuiya yetu,hiki ni kichwa sio mchezo.Madhumnuni makubwa ni kueleza watanzania wenzangu na kuelimishana kuwa tumefikia pabaya sana,mimi ni mtu mzima lakini hawa watoto wetu,vijana wetu wanaaibisha na kujiaibisha wenyewee!!!huku uraiani tunatembelea kurasa zao za Facebook na tunaona wanayoyaandika!na baadhi ya watu wanasifia kwa ujinga wao!wewe umekuja hapa kutukanana au maisha yako?na haswa wenye tabia hii ni akina dada!hivi mna nini nyinyi?kwakweli mnatia aibuuu!mnamuweka mtu picha yake!maelezo,matusi na mengineyo machafu hivi mnategemea nini?kumbukeni mnayoyafanya msione watu wananyamaza ila dawa yenu iko jikoni!kumbukeni hakuna mbio zisizo na mwisho!.Hivi nyinyi ni wasafi kiasi gani mpaka mnasema watu wengine?mnajua kisheria hii kitu ni kesi kubwa sana!mimi nimeishi hapa DMV kwa mika mingi lakini sijawahi kuona utumbo huu!!haohao wapigane harusini haohao matusi facebook unadhani utaheshimika?ni aibu kubwa sio kwa mwanamke tu hata kwa mwanaume na hata kwa vizazi vyako vijavyo!!!.naandika hii kwa uchungu mkubwa sana akina mama wa DMV mnasikitisha mnooo!nyinyi ndio wa kutegemea katika jamii yetu walezi na kila kitu lakini mnajidharaulisha!sasa mkitukana na kumdhalilisha mtu mnapata faida gani!!>Mimi nina mengi ya kusema,ila najua huwezi kumbadilisha mtu/mtoto wa mtu tabia yake ila kusema ni muhimu,na mnawatia aibu wazazi wenu na ndugu zenu,mimi kama mtanzania sijalifumbia macho hili limeniuma sana na naomba tushikane tuweze kuona jambo hili lifanywe vipi.Hili jambo ni kubwa sana na linaweza kuachiwa katika mkono wa sheria!poleni sana mliofanyiwa mambo haya na nawasifu kwa kukaa kimya ingawaje mlikua na uwezo na bado kuna uwezo wa kuwafikisha watu katika mikono ya sheria.Kwakweli mmevuka mpaka!na wala sio sifa na hawa mnaowatukana sio kwamba hawawezi kutukana,hawajui matusi ila wana adabu na wamelelewa vizuri walikotoka,nyinyi akina dada wote mnaotukana na majina yenu na background zenu tunazo mnasikitisha sana!hebu tuelezeeni kwenye hiyi facebook yenu kama nyinyi ni wasafi kuliko wengine kwa kiasi gani!sijawahi kuona mambo ya kipumbavu kama haya katika states zote hapa marekani ila hapa!hamuoni aibu!mwisho naomba watanzania wote tuone jinsi gani ya kusaidia hili balaa maa linaonekana ni tatizo sugu na hakuna kilichotendeka ndio maana bado wanaendelea!na tunaomba pia viongozi wa jumuiya yeu waliangalie kwa undani jambo hili,kwasababu kuna baadhi ya matusi pia yaliandikwa kwa mgombea mmoja wa chama lakini hakufanya action yoyote na sasa ni raisi wa jumuiya!kwanini ulilifumbia macho hilo swala!mpwa tafadhali itoe comment yangu hii japokua ni ndefu sana.Asante sana na endelea na kazi yako nzuri,usiyochagua wala kubagua.

Anonymous said...

Asante Mpwa aka Luka kwa kuwa mfano katika jamii sio tu katika kutupatia habari blogin lakini ata kuonyesha uzalendo wa kupiga kura Ata kama ulimchagua Loveness ilo ndo lilikuwa ni chagua lako na inabidi wana DMV tuli-respect na mimi binafsi sikuona kama ulinyea baadaya ya matokeo.pia nakubaliana na mdau wa juu kwamba wanawake wengine DMV di budi kuiga mfano wa DA loveness ni huyu ni dada shupave na ni jasiri.

Anonymous said...

Baadhi ya wanawake wenzetu DMV kwa kweli mnatia aibu na mnaipa DMV image mbaya. Wewe kama ukiwa mwanamke/mwanaume na pia mama/baba una mtoto/watoto huoni aibu kuandika matusi na mambo yasioyofaa waziwazi kwenye mitandao? Je mwanao/wanao wakija kuwa wakubwa wakasoma hayo mambo na wakianza kukudharau utasikitika au kujuta? Tumeshakuwa na familia wadada/wakaka wa DMV jamani tubadilike na kama sio kwa heshima yetu sisi wenyewe basi kwa heshima ya hawa watoto wetu na pia hata wadogo zenu. Ni aibu jamani, mwanamke unapendeza na kuvutia lakini tabia na maneno ni kama hauna wazazi. Hivi wazazi wenu wanayaona kweli haya na kama wanaona wanakubaliana nayo. Wengine wazazi wenu wapo hapa DMV inabidi waanze tena kuwafundisha maadili ili mtunze heshima za familia zenu. Watanzania tuungane na tuheshimiane tuko nchi za watu tunatakiwa tuishi kama ndugu wa kuzaliwa.

Anonymous said...

mpwa tunawataka watanzania wajuwe tunataka tuchukue sheria mkononi dmv kuna mtu lazima afatiliwe kisheria tupo pamoja