ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 16, 2012

Mwenyekiti wa UVCCM, mkoa wa Arusha James Millya ajiunga na CHADEMA leo

Mwenyekiti wa UVCCM, Mkoa wa Arusha, James Millya.
Na Gladness Mushi
MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa Arusha,kwa miaka mitano, James Millya, ametangaza kujiuzuru nafasi zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai kuwa CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.

Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye
Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini hapa.Alisema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.

Alitaja nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.
ALisema kuw ainasikitisha kuona Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa matamko kuwa Rais ajaye 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini na anayemfahamu ni Rais peke yake ambaye ni Jakaya Kikwete.
Millya alisema cha kusikitisha pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na hadi sasa Ikulu haijawahi kutoa kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza kauli hizo kutolewa, jambo lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kw anamna moja au nyingine na kauli hiyo.
Aidha alisema kuna Vijana wengi walioko ndani ya CCM wakiishi kwa matumaini ya kusubiri kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio Mkoa, ila yeye hawezi kuishi kwamatumaini kama muathirika wa Ukimwi.
Hata hivyo alitoa wito kwa Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi mema ya nchi yao, kumfuata Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la maisha ya watu.
Millya ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM tangu 2008 hadi sasa, aliwashukuru vijana kwa kumpa ridhaa hiyo na ataendelea kuwashukuru, ila ameamua kwa ridhaa yake kuachia ngazi zote kwa ajili ya ukombozi wa kweli. Millya hivi karibuni alijitosa kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge wa Afrika Mashari ndani ya Chama chake cha CCM, lakini alichinjiwa baharini na kutolewa jina lake.
Wakati Kiongozi huyo akitangaza kuachia ngazi hiyo ya juu ya UVCCM, ndani ya Chama cha CCM, Mkoa wa Arusha, Vijana mbalimbali wameonekana kutoamini walichosikia na wengi wao wakionyesha nia ya kumfuata.
CHANZO: HAKINGOWI.COM

3 comments:

Anonymous said...

Ameachia ngazi kwa sababu ya uroho wake wa madaraka baada ya kukosa nafasi ya kuwa mgombea wa ubunge wa Afrika Mashariki.. Millya acha unafiki wewe mwenyewe kwa maneno yako umesema kuwa hutaki kuishi kama muathirika.

Anonymous said...

Inawezekana ameachia ngazi kwasababu hiyo lakini pia si fair yeye amekifanyia kazi chama for all those years lakini wenye majina yao hawajafanya chochote wanakuja kuchukua fomu na kupeta kiulaini. It is just not fair! Hata hivyo namshangaa kwa uvumilivu wa ajabu toka kulipoanza kambi ndani ya chama yeye amekuwa mtu waku-fight lakini naona sasa chama hakibebeki tena kwa upande wa vijana.

Anonymous said...

ndio maana sinto kwenda chadema maana mtu akisha haribu wanakimbilia huko mimi nashangaa kwa nini mtu usibaki na chama ukibadilishe wewe unasema eti chadema ni beter