ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 9, 2012

Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ndugu Steven Charles Kanumba

Steven Kanumba katika picha ya pamoja na Saleh Mohammed

Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ndugu Steven Charles Kanumba
Ndugu Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii

Namwomba Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu na ustahamilivu kipindi hiki kigumu kwa sababu yote mapenzi yake itawachukua muda mrefu kumsahau mwenzetu ambaye alikuwa mtu wa watu, asiye na makuu licha ya umaarufu mkubwa aliokuwa nao.

Picha hapo juu nikiwa na ndugu yetu Marehemu Kanumba ilipigwa tukiwa katika mkutano wa watanzania kuingia katika mchakato wa kuandaa katiba na kuchagua viongozi watakao iendesha jumuiya ya watanzania waishio District of Columbia, Maryland na Virginia itakayokuwa imara, habari nyengine zilizopo pia kuna taarifa kwamba katika uchaguzi utakaofanyika jumapili ijayo, inasemakana tungelikuwa nae tena marehemu kanumba hapa marekani, lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu amemuita katika makaazi ya kudumu.


WOSIA
Watanzania tujaribu kufuata wosia aliotuwachia marehemu Kanumba watanzania tupendane.

Angalia clip yake marehemu hapo chini ambayo inakwenda sambamba na maneno yake.

No comments: