ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 9, 2012

TANGAZO MAALUMU LA MKUTANO WA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV TAREHE APRIL/15/2012

Ndugu Wanajumuiya,
Kama tulivyowafahamisha hapo awali kuwa kazi mliyotutuma imekamilishwa. Tuna washukuruni wote mlioleta na kutuma mapendekezo yenu kutokea mwanzo mpaka mwisho wa ukamilishaji wa Katiba mpya. Maoni yenu yote yalipokelewa na kufanyiwa kazi ndani ya Katiba, tunashukuru sana kwa mchango na muda wenu mliojitolea kwa nia ya kujenga Jumuiya yetu ya Watanzania DMV.
Hivyo basi, imetufikisha katika hatua kubwa naya mwisho ya kuindeleza mbele Jumuiya yetu. Na kama tunavyojua kuwa kwa sasa hivi hatuna Jumuiya na kamati iliyofanyia marekebisho katiba haina Fedha, Kutokana na hali hiyo, Wanakamati tumependekeza  kama ifuatavyo
-          Tutakuwa na Mkutano mkuu mmoja ambao utashughulikia maswala makuu mawili:

1.      Shughuli ya kwanza itakuwa ya kupitia na kupitisha Katiba.

2.      Shughuli ya pili itakuwa ya uchaguzi mkuu, tutachagua viongozi wa Jumuiya.

Mkutano Mkuu utafanyika tarehe  04/15/2012  saa 8 mchana ( 2:00pm).  Katika
Ukumbi wa  
MIRAGE HALL
1401 UNIVERSITY BLVD
HYATTSVILLE, MD 20783

3 comments:

Anonymous said...

is this have any thing to do with CCM?

Anonymous said...

This in a non political issue. It involves Tanzanians in the DMV regardless of their political affiliation. So it has nothing to with CCM or Republican parties.

Anonymous said...

Halafu ninyi viongozi wa DC waambieni watu hasa wale wenye kadi za kijani kwenda shule. Serikali ya Marekani ina mihela ya kuwalipia kila kitu jamani. Tutazidiwa na wanigeria mpaka lini? Mbona wenzetu wa state zingine wanasoma sana ndugu zangu? Tuache kununua jeans za $ 400.00 jamani. Twendeni shule wale wenzangu wote wenye kijani. Yaani mnanichefua, sijui mnataka mpaka nichue fimbo niwachape? Hata kama ujumbe huu utawauma, lakini najua ume-click.