ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 14, 2012

HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) IMEUNDA MKOA MAALUM WA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NA KUCHAGUA MAKATIBU WA MIKOA (9)


 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akielezea jambo wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeunda Mkoa Maalum wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kufanya uteuzi wa makatibu tisa wa mikoa. 
Taarifa iliyotolewa leo mjini Dodoma, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi Nape Nnauye imewataja Makatibu walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano kuwa ni wafuatao;-
1.     Ndg. Elikana Mauma               (Mkoa wa Mara)
2.     Ndg. Hilda Kapaya                  (Mkoa wa Geita)
3.     Ndg. Shaibu Akwilombe         (Mkoa wa Simiyu)
4.     Ndg. Hosea Mpagike               (Mkoa wa Njombe)
5.     Ndg. Alphonce Kinamhala     (Mkoa wa Katavi)
6.     Ndg. Aziza R. Mapuri              (Mkoa wa Magharibi)
7.     Ndg. Maganga Sengerema    (Atapangiwa kituo)
8.     Ndg. Adelina Geffi                 (Atapangiwa kituo)
9.     Ndg. Christopher Ngubiagai  (Mkoa Maalum wa Wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu)
           
Kuundwa kwa mkoa maalum wa wanafunzi wa elimu ya juu kunalenga kupanua wigo ikiwa ni mkakati wa chama kujiimarisha zaidi kwa wanachama wake wa kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu.
Uamuzi huu utawapa fursa wanafunzi wasomi ambao wengi wao ni vijana kupata fursa za kikatiba na kanuni kushauri na kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya ngazi ya juu katika chama cha Mapinduzi (CCM).

No comments: