ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 20, 2012

JK apata chakula cha jioni na uongozi DMV

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo May 20, 2012 alikaribisha kwa chakula cha jioni uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Washington na vitongoji vyake pamoja na wafanyakazi katika ubalozi wa Tanzania, katika hoteli ya Ritz-Carlton jijini Washington DC. 

Uongozi huo, kwa niaba ya wanachama wake, ulimpongeza Rais Kikwete kwa kuwa mmoja wa Marais wanne wa Afrika walioalikwa kwa mara ya kwanza katika historia kuhudhuria kikao cha nchi tajiri duniani zijulikanazo kama G-8 katika makazi ya mapumziko ya Rais wa Marekani ya Camp David, Maryland. 

Rais wa jumuiya hiyo Bw. Iddy Sandaly alisema kwamba mualiko wa kuhuduhuria mkutano wa G-8 alioupata Rais Kikwete umeendelea kudhihirisha kwamba mataifa makubwa yanaheshimu msimamo wake katika kuendeleza kilimo cha kisasa na kuondoa njaa duniani, ambavyo ndivyo vilivyokuwa kauli mbiu ya mkutano wa Camp David.

 Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na waziri wa kilimo Injinia Christopher Chiza pamoja na Waziri wa kilimo wa Zanzibar Mh Suleiman Othman Nyanga, pamoja na balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi Sinare Maajar. (Picha na Ikulu

 Sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo
 Rais Kikwete akiongea na uongozi wa jumuiya DMV
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akimshukuru Rais Kikwete kwa kuwaalika kwa chakula cha jioni

3 comments:

Anonymous said...

Tunaomba clarity hapa huu ni uongozi wa DMV au wote waliogombea uongozi wa DMV,maana nawaona hata wale waliogombea urais na ukatibu na hawakuchaguliwa na wao wapo kwenye picha hii! Ao mamcho yangu hayaoni vizuri??? Namwona dada loveness pembeni ya Rais na bwana Kinyemi?? hawa wanatuwakilisha DMV?? or ni private invites???

Anonymous said...

Pia namwona Kiongozi wa CCM Newyork, je na yeye anatuwakilisha DMV ?au ni private invitee?

Anonymous said...

Kuna Miraji nae kutoka Texas yeye kiongozi wa DMV? namwona pia Boyfriend wa Luvness!hebu tuelezeni vizuri jamani?