Mwandishi wa habari hizi alishuhudia majeruhi hao wakipatiwa huduma ya dharura kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni . Habari zaidi kutoka kwa maofisa waandamizi wa Jeshi na Polisi mkoani humu wamesema majeruhi hao walitarajiwa kusafirishwa usiku wa leo kupelekwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyekuwa tayari kueleza tukio hilo akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongela, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Fraser Kshaiu na Mkuu wa Kikosi cha 24 JWTZ, Mcheli ambao walienda eneo la mapambano.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, John Mongela aliwaambia waandishi wa habari kuwa Serikali itatoa taarifa ya tukio hilo baada ya kufanyika kwa kikao cha Kamati ya Ulinzi na usalama ambacho kinatarajia kufanyika leo.
Awali Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi katika mwalo wa Katonga, Mada Mussa alisema kuwa jumla ya mashine nane za boti na nyavu tatu ziliibwa na majambazi hao usiku wa kuamkia jana na ndipo wakatoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu tukio hilo.
Mada alisema kuwa jumla ya askari Polisi na wanajeshi 50 wanakadiriwa kushiriki katika kupambana na majambazi hao katika tukio lililotokea sehemu inayojulikana na wavuvi kama Msalabani.
Hata hivyo licha ya polisi na wanajeshi hao kujeruhiwa hakuna taarifa zozote rasmi za kukamatwa au kuuawa kwa majambazi hao.
Habari Leo
No comments:
Post a Comment