MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana ilimthibitisha Dk Milton Makongoro Mahanga (CCM), kuwa mbunge halali wa Jimbo la Segerea na Mahakama ya Rufaa Kanda ya Mbeya ikifanya hiyo kwa Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi, David Silinde (Chadema) baada ya kutoa hukumu ya kesi zilizokuwa zikiwakabili kwa nyakati tofauti.
Katika kesi ya Dk Mahanga, wafuasi wa Chadema, walimaliza hasira zao za hukumu ya kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo kwa kumzomea, Dk Mahanga baada ya Mahakama Kuu kumthibitisha kuwa ni mbunge wake halali. Dk Mahanga ameshinda kesi ya iliyokuwa ikimkabili iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa ubunge katika jimbo hilo kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kupitia Chadema, Fred Mpendazoe.
Hukumu ya kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2010, ilisomwa na Jaji Profesa Ibrahimu Juma huku ulinzi ukiwa umeimarishwa vya kutosha. Mapema asubuhi jana, kabla ya hukumu hiyo kusomwa, askari zaidi ya 50 walikuwa wametanda nje ya Mahakama ya Biashara, mahali kesi hiyo ilikokuwa ikisomwa.
Baadhi ya askari waliokuwa na virungu walilizunguka jengo hilo na wengine wakifanya doria kwa gari kuzunguka eneo la Mahakama hiyo kuhakikisha kuwa usalama ni wa kutosha. Mbali na askari hao waliokuwa na sare, pia kulikuwa na kundi la askari wengine waliokuwa wamevaa kiraia ambao nao walikuwa wakizunguka eneo la Mahakama hiyo wakati hukumu hiyo ilipokuwa ikiendelea kusomwa.
Ndani ya Mahakama Dk Mahanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, alifika mahakamani hapo mapema akiwa na gari la Serikali analolitumia kwa wadhifa wake huo. Akiwa amevalia suti nyeusi na tai nyekundu, alikwenda moja kwa moja kukaa katika benchi la mbele kabisa.

Akiwa ameketi kwa utulivu akisubiri jaji aingie, Dk Mahanga alikuwa anasoma gazeti na baada ya kumaliza alivaa miwani yake myeusi, kisha akatulia. Mpendazoe aliingia katika ukumbi huo saa 3:42 akiwa amevalia suti ya rangi ya kahawia na kukaa kwenye benchi la mbele upande mwingine tofauti na ule aliokuwa amekaa Dk Mahanga.
Wakili wake, Peter Kibatala alimfuata wakasalimiana, kisha akamkumbatia na baada ya kuachana na alimfuata mpinzani wake, Dk Mahanga wakasalimiana kwa kupeana mikono kisha wakanong’onezana jambo na baada ya hapo, Mpendazoe akarudi kukaa mahali pake. Ilipofika saa 3:59, Jaji Profesa Juma aliingia ukumbini na kukaa kwenye kiti chake.

Dakika mbili baada ya taratibu za kiitifaki kukamilika, alianza kusoma hukumu yake hadi saa 6:38, alipomaliza akizingatia hoja kumi na moja zilizokuwa zikibishaniwa na pande zote. Katika hukumu hiyo ya kurasa 79 aliyoisoma kwa lugha ya Kiswahili, Jaji Profesa Juma alitupilia mbali madai na maombi ya Mpendazoe akisema ameshindwa kuithibitishia Mahakama madai hayo kwa kiwango kinachotakiwa kisheria.
Alisema mlalamikaji alishindwa kuwaita baadhi ya mashahidi ambao wangeweza kuisaidia Mahakama katika madai yake, pamoja na vielelezo mbalimbali vya ushahidi kama ambavyo alikuwa ameeleza katika hati yake ya madai. Mashahidi hao muhimu ni pamoja na wale waliodai kumkamata Dk Mahanga na masanduku ya kura, badala yake mashahidi waliofika ni wale waliodai kuwa walisikia tu lakini hawakushuhudia tukio hilo.
“Kama ni kweli alikamatwa, ni kwa nini hata shahidi mmoja aliyeshiriki kumkamata asije mahakamani hapa kutoa ushahidi? Angetueleza walimkamataje na walimfikishaje Kituo cha Polisi Buguruni.
Huyu angetusaidia,” alisema Jaji Profesa Juma. Jaji alilinganisha na ushahidi wa utetezi uliokana Dk Mahanga kufikishwa kituo cha Polisi Buguruni akidai kuwa upande wa madai umeshindwa kuthibitisha zaidi ya kuwasilisha kielelezo cha gazeti tu. Mashahidi wengine ambao Jaji huyo alisema upande wa madai umeshindwa kuwaita ili kusaidia ni mawakala waliosimamia uchaguzi katika vituo mbali kuelezea kasoro mbalimbali alizoziibua Mpendazoe.
Kwa upande wa vielelezo, Jaji alisema upande wa madai umeshindwa kuthibitisha madai ambayo ni pamoja na mikanda ya video aliyodai inaonyesha tukio la Mtendaji wa Tabata kukamatwa na fomu za matokeo na mtu mwingine kukamatwa na mihuri ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Vielelezo vingine ni fomu za matokeo ya Ubunge namba 21B kuonyesha madai ya Mpendazoe kuwa ndiye aliyeshinda kwa kura 56,962 na Dk Mahanga akapata kura 44,904.
Lakini wadaiwa waliwasilisha fomu hizo ambazo Mpendazoe alidai 120 katika Kata ya Kiwalani na 129 Kata ya Vingunguti zilipotea na hazikujumlishwa, pia wakawasilisha fomu ya matokeo ya jumla (24B) ikionyesha Dk Mahanga alishinda kwa kura 43,554 na Mpendazoe kura 39,150.
Alisema Mpendazoe alishindwa kuwasilisha kielelezo chochote kuthibitisha madai yake kuwa ndiye aliyeshinda kwa idadi ya kura alizozitaja. Alisema wakati akihojiwa na Wakili wa Dk Mahanga, Jerome Msemwa mlalamikaji alishindwa kukumbuka kuwa alipata kura ngapi katika kila kituo katika Kata za Kiwalani na Vingunguti alikodai matokeo yalipotea. Jaji Profesa Juma alisisitiza kuwa Mpendazoe alipaswa kuwasilisha ushahidi thabiti vikiwemo vielelezo badala ya kudai kuwa alipata taarifa za makadirio kwa mawakala wake.
“Kutokanana na mapungufu hayo, naridhika kuwa mlalamikaji hakuiridhisha Mahakama kwamba kulikuwapo kwa ukiukwaji wa sheria katika mfumo mzima wa uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Segerea ulioathiri matokeo ya mwisho yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Novemba 3, 2010.”
“Hivyo ninaamuru kwamba Dk Milton Makongoro Mahanga alichaguliwa kihalali kuwa Mbunge wa Segerea, cheti kitatolewa kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuthibitisha kuwa alichaguliwa kihalali na mdaiwa wa kwanza, wa pili na wa tatu watalipwa gharama za kesi,” alisema Jaji Profesa Juma.
Kabla ya kufikia hitimisho hilo, Jaji Profesa Juma alichambua hoja kumi na moja zilizokubaliwa na mawakili wa pande zote kuwa ndizo zinazobishaniwa na ambazo zilihitaji kuthibitishwa huku akichambua ushahidi wa pande zote na kusema kuwa mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha madai yake hayo. Baada ya hukumu hiyo, Dk Mahanga aliwafuata Mawakili wake, Msemwa na Aliko Mwamanenge wakakumbatiana kwa furaha kabla ya kuondoka. Wakizungumzia hukumu hiyo, Mpendazoe na wakili wake walidai kuwa hawakuridhika wakidai kuwa Jaji hakuchambua vizuri ushahidi wa mashahidi wao.
Walidai kuwa kuna ushahidi mwingine wa mashahidi wao ambao Jaji ama aliuruka au hakuupa uzito. Wakili Kibatala alisema wameamua kukata rufaa kupinga hukumu hiyo na kwamba leo wanawasilisha mahakamani taarifa ya kusudio hilo. Licha ya Jaji kusoma hukumu hiyo kwa Kiswahili, ilidhihirika kuwa bado kuna wafuasi wengine wa Chadema ambao waliielewa kinyume.
Walidai kuwa pamoja na Dk Mahanga kushinda, Jaji amewaamuru mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na mdaiwa wa tatu, Msimamizi wa Uchaguzi (RO) walipe gharama za kesi. “Sasa kama Makongoro alishinda kihalali kwa nini awaamuru wengine walipe gharama za kesi? Hii si inadhihirisha kuwa walikiuka taratibu,?” alisikika mmoja wa wafuasi hao akihoji huku akiungwa mkono na wafuasi wengine.
Mpendazoe ilifungua kesi hiyo Novemba 10, 2010 akipinga ushindi Dk Mahanga akidai kuwa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi zilikiukwa katika hatua ya kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo. Baada ya hukumu Baada ya Jaji Profesa Juma kumaliza kusoma hukumu hiyo, kundi la wafuasi wa CCM wakiwa na bendera za chama chao walilipuka kwa shangwe wakiimba... CCM, CCM CCM.
Hata hivyo, shangwe zao zilifunikwa na kelele za wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wakiwazomea na kuwakejeli. Baadhi ya wafuasi wa Chadema walikwenda kwenye gari la Dk Mahanga na kuweka bendera ya chama chao kabla ya kuondoka eneo la Mahakama huku wakimzomea.
Silinde naye ashinda
Mahakama Kuu ya Rufaa Kanda ya Mbeya imeondoa kesi ya rufaa iliyokuwa inapinga uhalali wa ushindi wa Silinde iliyofunguliwa na Dk Lucas Siame wa CCM. Uamuzi huo ulitolewa jana na majaji watatu waliokuwa wakiisikiliza chini ya Mwenyekiti, Jaji Januari Msofe, William Mandia na Mbarouk S. Mbarouk baada ya wakili wa mlalamikaji, Victor Mkumbe kuwakilisha ombi la kutaka kuondoa shauri hilo mahakamani hapo.
Akiwasilisha ombi hilo mbele ya Mahakama hiyo ya Rufaa, Wakili Mkumbe alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya mlalamikaji kuonyesha nia ya kutotaka kuendelea na kesi hiyo huku akitumia kanuni ya 102 Kifungu cha Kwanza cha Kanuni za Mahakama Kuu ya Rufaa. Hata hivyo, Jaji Msofe alikikataa kifungu hicho kwa kusema kuwa kina upungufu na kisingeweza kutumika katika ombi hilo na badala yake kutumika Kanuni ya 4(2)(a) ya Kanuni za Mahakama Kuu ya Rufaa.
Katika kesi hiyo, Serikali iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu Mwandamizi, Obadia Kamea na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Rosemary Shio ambao waliridhia kuondolewa kwa rufani hiyo baada ya kuhojiwa na Jaji Msofe.
Jaji Msofe pia alimhoji wakili wa mlalamikiwa, Benjamini Mwakagamba baada ombi la mlalamikaji ambaye mbali ya kukubaliana na ombi hilo, aliitaka Mahakama kumwamuru mlalamikaji kulipa gharama.
Akisoma hukumu hiyo Jaji Mandia alisema Mahakama ya Rufaa imekubali ombi hilo na hivyo shauri hilo limeondolewa. “Kwa mujibu wa kanuni ya 4(2)(a) Mahakama inaliondoa shauri hili kutokana na pande zote kuridhia na inamwamuru mlalamikaji kulipa gharama zote alizotumia mlalamikiwa,” alisema Jaji Mandia.
Mara baada ya hukumu hiyo, Silinde alisema: “Mpinzani wangu ameshtuka na kujua kuwa nitamshinda na gharama za kunilipa zitaongezeka ndiyo maana amechukua uamuzi wa kuondoa kesi hii. Amefanya jambo la busara sana nampongeza.”
Kesi hiyo namba 24/2011 ilifikishwa Mahakama ya Rufaa baada ya Dk Siame kukata rufaa baada ya kushindwa katika kesi ya awali namba 2/2011 katika Mahakama Kuu chini ya Jaji Sophia Wambura.

No comments:
Post a Comment