ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 25, 2012

TANZANIA DMV KUKIPIGA NA MOROCCO, KESHO JUMAMOSI, GREENCASTLE

Timu ya kabumbu ya Watanzania DMV kesho Jumamosi May 26, 2012 itajitupa tena uwanjani kwenye Ligi ya DMV DIASPORA 2012 WORLD CUP mechi hii itachezwa saa 9 alasili juu ya alama kwenye uwanja uliopo Greencastle, Maryland (uwanja walioutumia kucheza na Ethiopia), uwanja # 5.

Mpaka sasa Tanzania DMV imeishacheza mechi tatu, imeshinda moja, imedroo moja na kufungwa moja.

Mechi iliyopita Tanzania DMV ilifungwa 2-1 na Portugal mechi iliyochezewa uwanja wa Heurich uliopo Hyattsville, Maryland na kilichopelekea timu hii kupoteza mchezo ni timu kucheza bila ushirikiano na baadhi ya wachezaji kucheza chini ya kiwango tofauti na mechi zilizopita.

Jabir Jongo amesema mechi ya kesho ni ngumu kwao kwani Morocco haijapomteza mchezo na tatizo lililojitokeza mechi iliyopita tumeishalifanyia kazi na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kimchezo leo Ijumaa tutafanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Heurich Hyattsville na kuhakikisha makosa yaliyotokea mechi ilyopiata yasiwepo.

Pia amesisitiza Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa nguvu vijana wetu pia napenda kuwashukuru mashabiki wote pamoja na wachezaji kwa mshikamano mnaouonyesha.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI DMV

No comments: