ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 2, 2012

WAKUU WA TAASISI ZA UMOJA WA MATAIFA (UN) WAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI.

 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk Alberic Kacou (kushoto), leo akihutubia Jukwaa la Wahariri aliwashakuru wahariri nchini kwa kazi kubwa wanayofanya katika utoaji wa taarifa za umoja huo. Amesema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusiana na shughuli za Umoja wa Mataifa ambalo pia limeenda sambamba maoni na taarifa zinazotolewa kuwa sahihi.
Dk. Kacou pia amesema kwa upande wa Umoja wa Mataifa, jitihada zimefanyika kuhakikisha kuwa masuala kutoka kwa waandishi yanapatiwa majibu kwa uharaka na urahisi. Moja ya jitihada hizo ni pamoja na uboreshwaji wa tovuti ya Umoja wa Mataifa Tanzania ambayo kwa sasa ina sehemu ya vyombo vya habari ambayo ni maalumu kwa kuhudumia mahitaji ya waandishi hapa nchini.
Mratibu huyo pia alilishukuru jukwaa la wahariri kwa kuonyesha nia ya kutaka kufahamu zaidi na kushirikiana na ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mipango yao ya ushirikiano na serikali ya Tanzania, bara na visiwani. Katikati ni Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen na Kulia ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot.
 Juu na chini ni Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot alisema Pamoja na utajiri mkubwa wa maliasili, Poimsot amesema kwamba Tanzania bado ina wananchi wengi sana ambao ni maskini. Amefafanua kwamba pamoja na pato la taifa limekuwa likiongeza kuanzia mwaka 2000, hali hiyo imekuwa ikitokea katika sekta ambazo haziongezi ajira kwa wananchi wa kawaida.
Pia ameelezia kwamba wananch wengi ambao wanapata fursa ya kuingia kwenye soko la ajira, mara nyingi inakuwa kwenye kilimo na sekta isiyokuwa rasmi ambapo uzalishaji pamoja na ujira unakuwa ni mdogo sana.
  Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen (wa pili kulia) amepongeza mafanikio katika kupanua elimu ya sekondari nchini na kusema kwamba mpango wa kuwa na angalau shule moja ya sekondari katika kila kata umefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Pia amepongeza mafanikio katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wengi zaidi wanajiunga na masomo ya sekondari na kwamba kumekuwa na usawa wa kijinsia katika uandishikaji wanafunzi shule za msingi.
Hata hivyo, Jensen, ameelezea masikitiko yake kwamba kadri wanafunzi wanavyoendelea na masomo ya juu sekondari usawa wa kijinsia umekuwa ukipungua. Amesema pia tatizo kubwa sio uandikishwaji wa wanafunzi mashuleni lakini ni kitu gani wanachojifunza.
Ameelezea kusikitishwa na kiwango cha elimu kinachotolewa nchini na kusema kwamba sio tu hakitoi uwezo wa kujiajiri kwa wanaomaliza sekondari, bali pia kinatoa fursa chache kwa wanafunzi kuendelea na masomo ya juu.
 Mkurugenzi wa UNAIDS Tanzania Dr. Luc Barrier (kushoto) amefafanua kwamba mapambano yatayoweza kuzaa matunda dhidi ya UKIMWI katika nchi ni yale ambayo yatahusisha sekta zote za jamii. Alisistiza kwamba kaasisi taasis iliyopo chini ya Umoja wa Mataifa, shughuli zao zinaendeshwa sambamba na sera za nchi husika katika masuala ya kupambana na UKIMWI.
Dr Barrier amesema kwamba jamboa la kwanza ambalo hulifanya kama taasisi ni kuangalia hali halisi ya nchi, vipaumbele vya serikali husika na ndipo hufikia maamuzi ya kukutana na wahusika kutoka upande wa serikali ili kuweza kufahamu Umoja wa Mataifa wanaweza kuchangia na kusaidia vipi katika mipango na sera ya nchi.
Ameongeza kwamba ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na serikali ya nchi husika umekuwa na mafanikio kwa sababu hausishi sekta ya umma pekee bali na sekta binfansi katika kutasfiri mikakati na mipango ya kupambana na UKIMWI.Katikati ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou, Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen na Kulia ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot.
Msaidizi Mshauri wa Umoja wa Mataifa Bw. Tobias Rahm akijumuisha katika mkutano wa taasisi za Umoja wa Mataifa na Jukwaa la Wahariri, Rahm alisema kwamba ni matumaini yake kuwa vyombo vya habari vitaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi katika kuongea ufanisi na uelewa wa shughuli zao.  
                                                                         (Picha kwa hisani ya MO Blog)

No comments: