![]() |
| Waziri mpya wa Fedha, Dk. William Mgimwa |
Waziri mpya wa Fedha, Dk. William Mgimwa, amesema kazi yake ya kwanza katika wadhifa huo ni kushughulika na mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa sarafu ya Tanzania inalindwa dhidi ya matumzi ya ovyo ya Dola ya Marekani.
Katika mahojiano maalum na NIPASHE mjini hapa juzi, Waziri Mgimwa, alisema mfumuko wa bei ni tatizo na ni lazima kujipanga upya katika kuimarisha mifumo ya kiuchumi nchini.
“Mfumuko wa bei ni tatizo na namna ya kulitatua hili ni kuimarisha baadhi ya mifumo ikiwamo kuziboresha sera tulizonazo na kuuza zaidi bidhaa zetu nje ya nchi badala ya kuingiza, lakini pia ni lazima tuhakikishe tunaimarisha misingi ya uzalishaji wa chakula,” alisema Dk. William Mgimwa ambaye pia ni Mbunge wa Kalenga.
Dk. Mgimwa alisema juhudi hizo ni lazima ziende sambamba na mikakati ya kulinda thamani ya sarafu ya Tanzania ambayo imekuwa ikiporomoka thamani yake mfululizo.
“Kwa mfano huu mfumuko wa bei tulionao hivi sasa ambao umesababisha kupaa kwa gharama za maisha kunakoligharimu taifa kwa sasa, huko nyuma kulichangiwa na serikali kuchelewa kupeleka fedha za ununuzi wa chakula cha akiba katika maghala ya taifa,” alisema.
Alisema hali hiyo ndiyo imechochea mfumuko wa bei kutokana na kuadimika kwa baadhi ya vyakula sokoni kwani usambazaji wake umekuwa mdogo tofauti na mahitaji ya nchi.
Kwa mujibu wa taarifa Ofisi ya Takwimu Taifa (NBS) iliyotolewa Jumanne wiki hii, mfumuko wa bei kwa Aprili ulishuka hadi asilimia 18.7 kutoka asilimia 19.0 za Machi mwaka huu.
Taarifa ya NBS pia ilionyesha kuwa vyakula vilichangia ongezeko la bei hizo kwa mchanganuo kwamba; mchele asilimia 3, mahindi asilimia 1.6, unga wa mahindi asilimia 0.5, vitafunwa asilimia 7.3, unga w amihogo asilimia 6.7, mayai asilimia 2.1, siagi asilimia 2.9, machungwa asilimia 6.8, ndizi mbivu asilimia 4.8, maembe asilimia 12.8, papai asilimia 8.9 na nanasi asilimia 8.7.
Vyakula vingine na asilimia za kupanda kwa bei kwenye mabano ni mbogamboga (2.2), mihogo (7.7), vinywaji baridi (9.7); wakati bidhaa zisizo za chakula ni mavazi (0.9), gesi (3.9), mafuta ya taa (2.3), mkaa (5.3), petroli (3.9), na begi z amikononi (5.6).
Wakati mfumuko wa bei ukionyesha picha hiyo, NBS pia ilisema kuwa kuanzia Septemba 2010 hadi Aprili 2012 Shilingi imepoteza thamani yake kwa wastani wa asilimia 22.75, kwa maneno mengine Sh. 100 ya Septemba 2010 sasa thamani yake ni Sh. 77.25.
Waziri huyo pia alisema taifa linaweza kukabiliana na tatizo la mfumuko wa bei, kwa kuwa na utaratibu bora zaidi wa kuuza bidhaa nyingi zaidi nje ya nchini kuliko kuingiza, na kuna haja ya Wizara yake kujipanga na kuhakikisha kwamba inakuwa na sera nzuri ambazo zitachangia katika kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.
Bila kutaka kukosoa utendaji wa Waziri aliyetangulia, Mustafa Mkulo, Dk. Mgimwa alisema: “Taifa limetumbukia katika mfumuko wa bei kwa sababu serikali huko nyuma ilichelewesha kupeleka fedha kwenda kwenye maeneo yenye maghala ya taifa yanayonunua chakula.”Alisema kuwa hali hiyo haitaachwa itokee tena.
Alisema mkakati mpya wa kuokoa thamani ya Shilingi ni kuhakikisha kwamba matumizi yote ya fedha na mahitaji ya nchi yanafanyika kwa fedha za Tanzania badala ya Dola ili kuliepusha taifa kuendelea kuathiriwa na hali hiyo.
Waziri huyo ambaye anakabiliwa na kibarua kikubwa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao cha kuwasilisha bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 bungeni hapo Juni, alisema amejipa malengo ya kupitia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ya mwaka 2009/10 ambayo iliwasha moto bungeni hadi kusababisha mawaziri sita kupoteza kazi na naibu mawaziri wawili, ili kuimarisha mifumo ya kiutendaji wizarani hapo.
Hiki kitakuwa ni kibarua kikubwa cha Dk. Mgimwa kubadili sura ya Hazina ambayo katika miaka ya hivi karibuni imekabiliwa na tuhuma mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuchukua hatua zozote za kukabiliana na mfumuko wa bei, kuyumba kwa thamani ya Shilingi, lakini pia serikali ikituhumiwa kuruhusu matumizi ya ovyo kabisa ya fedha za walipa kodi.

CHANZO: NIPASHE
.jpg)
1 comment:
Inaonekana utafanya kazi nzuri ya wananchi Dr.
Usituangushe Watanzania wana imani nawe.
Post a Comment