Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Mkewe, anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na Mumewe, Profesa Cleophas Migiro wakisubiri kusalimiana na wageni waalikwa wakati wa hafla ambayo Ban Ki Moon aliandaa maalum kwajili ya kumuaga msaidizi wake wa Karibu.
Ban Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo amempogeza na kushukurusu sana Migiro kwa namna alivyokuwa mshauri wake na mwalimu wake ambaye a anasema kwa ualimu wake anampa alama ya plus plus plus. akatumia hafla hiyo kutangaza kwamba anamteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika. Migiro anaondoka baada ya kuutumikia Umoja wa Mataifa kwa miaka mitano na nusu.
Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa hafla hiyo, akatoa shukrani zake kwa Ban ki Moon kwa kumpatia heshima hiyo ya kihistoria ambayo haita kaa ifutike na kwamba ameupokea uteuzi huo kwa mikoni miwili na hasa kutokana na kwamba tatizo la ugonjwa wa ukimwi ni tatizo ambalo analichukulia kwa uzito wa aina yake.
Profesa Migiro akiwa na Bint yake, Chansa- Jasmin wakifuatilia hafla hiyo kwa makini
.Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Bi. Munanka akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon anayetazama ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro
Sehemu ya wageni waalikwa
Na Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,
amemteua Naibu Katibu Mkuu anayemaliza
muda wake, Dkt, Asha-Rose Migiro kuwa
mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani
Afrika.
Ban Ki Moon ametangaza uteuzi huo wakati wa hafla
maalum aliyoiandaa mahsusi kwaajili ya kumuaga
Naibu Katibu Mkuu wake,ambaye anahitimisha utumishi wake wa miaka mitano na nusu katika nafasi ya Unaibu katibu Mkuu.
Hafla hiyo imefanyika
siku ya alhamisi katika viunga vya Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na
wageni waalikwa mbalimbali wakiwamo mabalozi
na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“Ninatangaza rasmi kwamba ninamteua dkt. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wangu maalum katika masuala ya ukimwi
na ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika.
Akasema Ban Ki Moon tangazo
lililoshangiliwa kwa nguvu na wageni waalikwa.
Akiongea kwa hisia, Ban Ki Moon, ameeleza kwamba
ingawa Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wake, lakini amekuwa mwalimu wake,
amejifunza mengi toka kwake na daima ataendelea kuenzi mchango wake mkubwa.
“ Kama ni kuvaa viatu vyake, naweza kusema
ningechekesha sana, kwa ufupi siwezi
kuvaa viatu vya Migiro, amekuwa msaada mkubwa sana kwangu, ameniwakilisha vema
kila mahali nilipomtuma hata katika
mazingira magumu na ya hatari, kote
ameniwakilisha vema sana, kama mwalimu
wangu, na kama profesa wangu anastahili alama ya juu sana” akasema Ban Ki Moon na kushangiliwa.
Akamuelezea
Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini mwanadiplomasia aliyebobea, aliyefanya kazi kubwa,ngumu na
nzito kwa moyo mkunjufu, uhodari , umakini, na uadilifu wa hali ya juu sana.
“ Siyo rahisi
kuelezea yale aliyoyafanya nyuma ya pazia, namna gani alivyochapa kazi kwa
nguvu, yapo mengi makubwa ambayo Migiro
ameyafanya na kuyakamilisha kwa uadilifu
wa hali ya juu. Migiro ni mwanadiplomasia aliyebobea lakini ni mtu wa vitendo,
vitendo ambavyo lazima utaona matunda yake” akabainisha Ban Ki Moon
Na kuongeza “
Migiro amefanya kazi na viongozi
wagumu, kiwamo aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Quadaff aliyethubutu hata kumrushia katiba ya
Umoja wa Mataifa, amezikuna nyonyo za watu wengi wakiwamo watu wanyonge na
wenye matatizo mbalimbali. Migoro
unaondoka, lakini Umoja wa
Mataifa hauta sahau mchango wako.
Hapa ni nyumbani kwako, na nitaendelea kuomba msaada wako na ushirikiano wako, bado
nitaendelea kukuhitaji” akasisitiza Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, akatumia fursa hiyo
kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kumruhusu Migiro kwenda kuitumikia jumuia
ya kimataifa.
“ Ninapenda
kutoa shukrani zangu za pekee kwa
jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kumtoa Migiro katika utumishi wake
wa Umma kuja kunisaidia , kwa serikali ya Tanzania na watanzania nasema asanteni sana” akasema Ban
Ki Moon..
Kwa upande wake,
Naibu Katibu Mkuu dkt. Asha-Rose Migiro amesema anaupokea kwa mikono miwili
uteuzi wa kuwa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu katika masuala ya Ukimwi.
Akasema masuala ya
ukimwi na ugonjwa wa ukimwi, ni eneo ambalo limo ndani ya moyo wake na kwamba anashukuru kuona kwamba Katibu Mkuu
anamuamini kwamba anaweza kumsaidia. Akaahidi kwam atalitekeleza jukumu
hilo kwa heshima kubwa.
Akamshukuru Ban Ki
Moon, kwa kumuamini kwamba anaweza kumsaidia kama naibu Katibu Mkuu, na
akamshukuru pia kwa ushirikiano mkubwa na uhusiano mkubwa uliojengeka kati yake
na Ban Ki Moon lakini pia kati yake na wasaidizi wake. Ushirikiano ambao anasema ulichagiza utendaji kazi kufanikisha dira na matarajio ya Katibu Mkuu.
“Katibu Mkuu amenipa heshima ya kihistoria, heshima ya
kuwa msadizi wake, ni heshima kubwa
kwangu na kwa yeyote atakayekuja kuandika historia yangu, kwa namna yoyote ile
hawezi kukwepa kumtaja Ban Ki Moon, naomba nikushukuru sana kwa
heshima hii kubwa uliyonipa” akasema Migiro.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na familia ya Naibu Katibu Mkuu
ikijumuisha mume wake, Profesa Cleophas Migiro, mdogo wa
Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina
Mtengeti na mtoto wa mwisho wa
Migiro Chansa Jasmin.
Naibu Katibu Migiro anakuwa mwanamke wa pili kushika
wadhifa huo na mwanamke mwafrika wa kwanza. Lakini pia ni naibu katibu mkuu
ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.
No comments:
Post a Comment