Tuesday, June 5, 2012

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Steve Kilindo (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw Raymond Mushi, msaada wa vifaa vya usafi kwa ajili ya Manispaa ya Ilala, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, Dar es Salaam jana. (Na Mpigapicha Wetu)
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Zantel Bw Ahmed Mokhles akionesha katika runinga moja ya huduma mpya ya Epiq Moto kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam juzi, huduma itakayowawezesha wateja kupiga simu kwa mitandao yote kwa Sh.1 kwa sekunde kwa saa 24 na kutuma sms kwa Sh. 25, pia mteja wa kampuni hiyo atapewa megabaiti 50 za intaneti bila malipo. (Picha na Charles Lucas)
Mwenyekiti wa Chama cha Kupambana na Dawa za Kulevya na Ulevi, Tanzania (IOGT), Bw. Mohamed Lichonyo (kushoto) akizungumza na vijana wa chama hicho kutoka Shule ya Sekondari Tuliani Kinondoni walipowatembelea vijana wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ili kujifunza shughuli za ulinzi shirikishi polisi jamii. 
(Picha na Charles Lucas)
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Sophia Simba (aliyeketi) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari, walipokutana kwenye Kamati za Bunge zinazoendelea, Dar es Salaam jana. (Picha na Peter Mwenda)
Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Bi. Juanita Mramba (aliechuchuma katikati) akiongoza wafanyakazi wa benki hiyo kupanda miti katika Kata ya Kivukoni wakati wa kuazimisha wiki ya mazingira Dar es Salaam jana. (Na Mpigapicha Wetu)
Wafanyakazi wa Exim Bank wakichangia damu salama jana, jijini Dar es salaam.
(Picha na Mpigapicha wetu)
Picha kwa hisani ya majira

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake